WAZAZI WASHAURIWA KUTOWAFUNGIA WATOTO WENYE ULEMAVU NDANI

 


Wazazi washauriwa kutowafungia watoto wenye ulemavu ndani. 

Na Suzana Alex

Wazazi  wameshauriwa kutowafungia watoto wenye ulemavu majumbani badala yake wawapeleke shuleni wapate elimu kwani watoto hao wanafaida kwa familia na serikali. 

Veronika Mrope ni Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Nala ilyopo Jijini Dodoma akizungumza na wazazi,wadau wa elimu na watendaji wa kata kwenye mahafali ya wanafunzi wa darasa la saba yaliyofanyikia katika viwanja vya shule hiyo septemba 17,amesema ni muhimu wazazi kuhakikisha wanawapatia watoto elimu kwani wote ni sawa. 

Amesema ni jukumu la wazazi kuhakikisha wanawasimamia watoto wao katika masomo yao ili kuepuka utoro unaojitokeza na kupelekea watoto hao kutokumaliza masomo yao.

"Niwaombe ushirikiano wazazi shule yetu Ina wanafunzi 40 wenye uhitaji lakini baadhi ya wazazi wanaficha watoto wenye ulemavu  ndani si jambo jema. 

"Mimi ni mdau mkubwa wa elimu naumia kuona wazazi hawawasimamii watoto wao kwenye elimu watoto wengine ni watoro Hali inayopelekea kutokumaliza  masomo Yao hawa watoto tusipowasimamia Leo huko mbeleni tutahangaika sisi wenyewe,"amesema Mrope

Kwa upande wake mwanafunzi wa  shule hiyo alipokua akisoma risala Mwajuma Bilali alibainisha kuwa shule hiyo inauhitaji wa vifaa vya kitehama kama vile mashine za kutolea nakala maalumu(photocopier machine),kompyuta na vifaa vingine,uhaba wa viti na meza pamoja na kuomba kuchimbiwa kisima shuleni hapo.



Naye Projest Amos meneja masoko kiwanda cha mbolea ITRA COM aliyekua mgeni rasmi alipokua akijibu risala hiyo  aliahidi kushirikiana  shule hiyo kwa kutoa misaada mbalimbali inayohitajika

Hata hivyo amewaomba wakazi wa eneo Hilo wanaofanya kazi katika kiwanda hicho kutojichukulia likizo zosizokua na maana baada ya kupata mshahara.



Post a Comment

Previous Post Next Post