MGOMBEA UDIWANI KATA YA MAJENGO CCM AHAIDI KUSHIRIKIANA NA WADAU KULETA MAENDELEO

 


Na Suzana Alex

MGOMBEA Udiwani kata ya Majengo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Nicolaus Msemo amesema akipitishwa kwnye nafasi hiyo ya udiwani atashirikiana na wadau wa maendeleo na serikali ili kuondoa kero zilizodumu kwa muda mrefu ikiwemo wa uchakavu wa majengo ya shule ya msingi Kaloleni ambayo iliyojengwa toka utawala wa mkoloni.



Aidha kero zingine ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara na uwekaji wa mifumo mipya ya maji taka ambayo imekuwa kero kwa wakazi wa kata hiyo kwa kipindi kirefu hivi sasa.

Msemo amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kata hiyo kwenye mkutano wake wa kujinadi uliofanyika katika uwanja wa stendi ya daladala ya majengo Jijini Dodoma. 

Amesema ili kuondoa kero hizo anaomba kuchaguliwa na kwa pamoja kwa  kushirikiana na wadau wa maendeleo na wananchi naamini kero hizo zilizodumu kwa miaka mingi itaweza kutatuliwa.

Akizungumza na wananchi hao alisema uboreshaji wa upatikanaji wa mikopo inayotolewa na Halmashauri ya Jiji kwa makundi maalumu ya akina mama,vijana na watu wenye ulemavu watapatiwa elimu ya mafunzo ya biashara ili fedha hizo watakapozipata waweze kunufaika nazo 

Amesema pamoja fedha hizo zinatolewa na Halmashauri lakini changamoto iliyo ni namna ya kutambua matumizi na ndiyo maana walio wengi wanajikuta wakifilisiwa na kujikuta wakiingia kwenye mikopo ya kausha damu.

"Mafanikio ya yote haya yatawezekana kwa pale wananchi,wadao wa maendeleo na serikali tutakapounganisha nguvu kwa pamoja na hatimaye kero hizo zinaweza kuondoka na sivyo vinginevyo"alisema.



Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Charles Mamba amewataka wale wote waliotia nia ya kugombea nafasi ya udiwani kwenye jimbo la Dodoma waungane na waliopitishwa na chama hicho ili ushindi wa kutosha upatikane kwa malengo ya kuleta maendeleo.

Mamba amesema kuwa hakuna haja sasa ya kuwepo kwa makundi ndani ya chama,kinachotaki ni kuungana kwa pamoja kwa lengo la kukipa ushindi chama na watanzania waweze kunufaika na maendeleo yaliyopo.

Post a Comment

Previous Post Next Post