Mgombea udiwani zuzu aomba ushirikiano ili kuleta maendeleo
Na Suzana Alex
Mgombea Udiwani mteule kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Zuzu Jimbo la Dodoma mjini,Jenesta Malingo amesema atahakikisha anawaondolea
wanafunzi adha ya kutembea umbali mrefu kwa kufuatilia usajiri wa shule ambao haujakamilika.
Akizungumza na wananchi wa kata hiyo kwenye mkutano wa kujinadi uliofanyikia katika mtaa wa Chididimo Septemba 14,amesema wanafunzi hutembea umbali mrefu takribani km16 kwa siku kwenda na kurudi jambo ambalo linapelekea usalama wao kuwa mdogo zaidi.
"Shule ipo imekwisha jengwa,madarasa yamekamilika na walimu wapo jambo linalopelekea wanafunzi kutembea umbali mrefu ni usajiri wa shule ambao haujakamilika nikiingia madarakani jambo la kwanza kulifanyia ufumbuzi ni kufanya hatua zote za kiusajiri ili kuwapunguzia mwendo watoto wetu.
Aidha amesema kwa kushirikiana na wananchi na wadau wa maendelea wataongeza miundombinu mbalimbali kwa kuijenga ikiwemo ya maji,na kujenga vituo vya afya ambavyo vitasaidia kina mama nyakati za kujifungua pamoja na kusimama kuimarisha uchumi wa wananchi wa kata hiyo.
"Nitasimama imara katika mabaraza ya madiwani kwa ajili ya kuongelea hali ya uchumi wa wananchi wetu kwa maana ya kwamba ile asilimia 10 ya mikopo inayoenda kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu inawafikia wananchi bila upendeleo wa aina yoyote ,"
amesema malingo
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa kata hiyo Omary Kagusa amewataka watia nia wa Udiwani ndani ya kata hiyo kuacha makundi na kushirikiana ili kupata ushindi
"Ikiwa sisi wenyewe hatuelewani itatoa nafasi ya wapinzani kupata nguvu zaidi sasa ni wakati wa kuungana na kutafta kura kwa kishindo makundi sasa yamefika mwisho," amesema



Post a Comment