Wananchi wa kijiji cha Mwakalima kata ya Kanyelele Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wameipongeza Serikali kwa kuwapatia Hakimiliki za Kimila hatua inayowafanya kumiliki maoneo yao kihalali.
Wananchi hao wamebainisha hayo Septemba 11, 2025 kwa nyakati tofauti mara baada ya kukabidhiwa Hakimiliki za Kimila.
Zoezi hilo limehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Bi.Johari Samizi, Afisa Ardhi Mteule Wilaya ya Misungwi Bi. Florida Busheli na Michael Sambu Mkurugenzi wa kampuni ya Kupima ardhi (GMS) GEOTECH CONSULTANCY CO LTD ambayo inashirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi katika zoezi hilo.

Post a Comment