TRA YAANZISHA DAWATI MAALUM KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA.

 


Na Suzana Alex

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule amewataka wafanyabiashara kulipa Kodi stahiki kwa kujenga mazingira yenye uwazi ili kuendelea kuongeza pato la taifa na kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumza  wakati wa uzinduzi wa dawati maalum la uwezeshaji biashara la Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA)

katika viwanja vya Nyerere square Jijini Dodoma septemba 11, amesema wananchi wanatakiwa waombe risiti na wafanyabiashara watoe risiti. 

"nafahamu wafanyabiashara wadogo wadogo wanapokua wengi ndipo Kodi inaongezeka  ni heri watu wengi wanaotoa kidogo kidogo kuliko mtu mmoja anaetokea kikubwa ikitokea akafunga biashara yake hatutoweza kupata Kodi," amesema Senyamule

Aidha ametoa wito kwa wananchi kujitokeza Oktoba 29 kwaajili ya kupiga kura kwasababu ni jambo la lazima na la kikatiba.

Kwa upande wake  Kamishna Mkuu wa mamlaka ya mapato nchini Yusuph Mwenda,amesema dawati hilo litawafikia wafanyabiashara na kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo na kupelekea biashara zao kufa.

Amesema hivi karibuni wataingia makubaliano na SIDO ambao watashirikiana na TRA kuwezesha viwanda vidogo vidogo viwepo  jijini hapa na watatumia 4R za Rais ili kuendelea kukusanya kodi. 

"Sisi kama TRA kwa niaba ya serikali ni washirika wenu katika biashara zenu biashara mnazoanzisha ni za kwetu pia kwasababu zikikua baadae zitasaidia maendeleo ya nchi zisipokua,zikifa hamtaendelea kuchangia maendeleo ya nchi ili muendelee kuchangia maendeleo ya nchi ni lazima kama TRA tushiriki na nyie wakati mnaanzisha biashara zenu tuwasaidie kwa kuwatambua,kuwasikiliza na kuwawezesha ili biashara zenu zikue na mkifika level kubwa muanze kuchangia na mkichangia ndio mnachangia nchi yetu inaendelea.

 "Kwetu sisi Kodi ni akili ya kwanza ni biashara hakutakua na Kodi kama hakuna biashara na ndio maana tumeanzisha dawati kwa ajili kuwatambua ili tuwasikilize mna shida Gani tunawezaje na sisi kushiriki kutatua changamoto zenu,tunawasaidiaje mkue kazi ya dawati hili ni kushirikiana na taasis zingine," amesema Mwenda

Hata hivyo Kamishna huyo ametembelea baadhi wa wafanyabiashara na kusikiliza changamoto wanazokumbana nazo kubwa ikiwa ni kukosekana kwa ushirikiano baina ya taasis tofauti.

Post a Comment

Previous Post Next Post