MGOMBEA UDIWANI KATA YA BUIGIRI AHAIDI KUBORESHA MIUNDOMBINU

 


Mgombea udiwani kata ya buigiri ahaidi kuboresha miundombinu

Na Suzana Alex

Mgombea Udiwani Mteule kupitia  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Buigiri Jimbo la Chamwino Kenneth Yindi ahaidi kuboresha miundombinu na kusimamia miradi ijayo kwa utaratibu maalumu.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa kujinadi uliofanyikia katika viwanja vya Chinangali II Septemba 10 amesema ili kata hiyo iendelee inahitaji ushirikiano baina yake na wananchi  kutatua changamoto zilizopo.

"Naenda kutatua changamoto ya chakula shuleni kwa ushirikiano wa wazazi,walimu na wananchi mbalimbali hilo sisubiri chochote lazima litatuliwe ili wananchi wenye uwezo tofauti  wale chakula shuleni kazi yao ni kusoma tu mipango ninayo utaratibu ninao nitawashirikisha labda nyie mkatae lakini Hilo lazima nilitatue ili mtoto kazi yake iwe ni kwenda shuleni asifukuzwe shuleni kwa sababu ya chakula.

"Mimi nitakua kiunganishi kati ya serikali na wananchi matatizo yenu nitayapeleka kwa mbunge  yanayowezekana ndani ya kata yatafanyika Kuna mengine tunayafanya sisi wenyewe kwa ushirikiano 



Aidha amewataka vijana kuepuka mikumbo ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii kwani inahatarisha amani ya nchi.



Kwa upande wake aliyekua mtia nia wa ubunge Jimbo la Chamwino ndani ya chama hicho amehamasisha kina mama kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi ili kupiga kura 

"wakina mama ni jeshi kubwa niwaombe tarehe 29 itakapofika saa11 asbuhi amka uwahi kupanga foleni,"amesema Kayombo



Post a Comment

Previous Post Next Post