Kikosi cha Timu ya Mamelodi Sundowns ya South Africa kimewasili Dar es salaam kwa ajili ya kucheza mechi yao ya kwanza ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Yanga siku ya Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Mamelod wamewasili Tanzania wakiwa na vyakula na vinywaji vyao ambavyo kutokana na kuonekana kutoenea kwenye sehemu ya mizigo ya Basi lililowapokea, imebidi vibebwe kwenye gari la mizigo aina ya cante.


Post a Comment