WATU 12 MBARONI KULA MCHANA HADHARANI ZANZABAR

 Kufuatia taarifa mbalimbali zilizosambaa mitandaoni zikidai kuna baadhi ya Watu Visiwani Zanzibar wana tabia za kula chakula hadharani wakati wa mchana mwezi huu wa Ramdhani, Jeshi la Polisi limefuatilia taarifa hizo na kubaini uwepo Watu hao.



Kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa mjini magharibi (Zanzibar) amesema walifanya msako na kuwakamata Watu hao 12 katika maeneo tofauti ya mjini ambapo sasa wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Madema wakisubiri taratibu za kupelekwa Mahakamani.



SEMA TV hapo awali kabla ya kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani ilifanya mahojiano maalum na Mrajisi wa Baraza la Sanaa Zanzibar ambalo pia husimamia Milka, Silka na Tamaduni za Zanzibar na ambapo alizungumzia kanuni zinazopiga maarufuku mbalimbali za mwezi mtukufu ikiwemo kusimamisha shughuli za mziki, kufungua Baa, ulaji holela wa hadharani na uvaaji usio na staha. 

Post a Comment

Previous Post Next Post