Vongozi wa klabu ya Simba umepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali za mashabiki wetu zilizotoke usiku wa kuamkia leo wakiwa njiani kuelekea Dar es Salaam kushuhudia mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.
Ajali ya kwanza imehusisha mashabiki wa Tawi la Kiwira Rungwe la mkoani Mbeya ambapo imetokea katika eneo la Vigwaza, Pwani.
Taarifa za awali kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza mtu mmoja amepoteza maisha.
Ajali ya pili ni Tawi la Wekundu wa Border kutoka Tunduma iliyotokea Doma, Mkoani Morogoro. Taarifa kutoka eneo la tukio inaeleza kuwa mtu mmoja ameumia na hakuna madhara makubwa.
Tayari viongozi wa Simba wanaelekea eneo la ajali Vigwaza ili kutoa msaada zaidi kwa waathirika. Uongozi unatoa pole kwa wote walioathirika na ajali hizo, familia pamoja na Wanasimba wote kwa ujumla.


Post a Comment