MIKOPO YATAKIWA KUHESHIMIWA NA SI KUOGOPWA

 



Na Suzana Alex 


Wananchi wahamishwa kuchukua mikopo na kwenda kuifanyia jambo lililokusudiwa kwani kwakufanya hivyo kutaepusha wao kutoingia migogoro na taasisi zitoazo huduma hiyo.


Abdallah Salum ni Meneja benki ya ushirika tawi la Dodoma amesema mikopo si ya kuogopa bali inatakiwa kuheshimiwa.


Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa tatu wa mwaka na chama cha ushirika wa akiba na mikopo, Dodoma Women Saccos(DOWOSA)amesema benki ya ushirika inakopesha saccos na saccos inakopesha wanachama wake.


"Mikopo sio ya kuogopa unachotakiwa ni kuiheshimu kinachotakiwa usichukue mkopo kwenda kuifanyia jambo lingine bali lililokusudiwa. 

"Sisi tunawapatia ukwasi na wao wanawakopesha wanachama wao pia saccos inatakiwa iwe na miradi kwakua miradi ni kitu muhimu,"amesema Salum 


Kwa upande wake Denis Nguruse ambaye ni Afisa Ushirika mkuu kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania(TCDC)amesema saccos nyingi nchini hazina rasilimali bali hukopa kupitia mali za wajumbe


"Kwenye vyama vya ushirika huwa hatutengenezi faida ila tunatengeneza ziada mara nyingi tunapenda kutengeneza ziada ili kumsaidia mwanachama,"amesema Nguruse


Naye Mwenyekiti wa Dodoma Women Saccos(DOWOSA)Kitolina Kippa amewakumbusha wanachama wa Saccos hiyo kuendelea kuweka akiba ya kutosha ili kupata mkopo mkubwa


Chama hicho kilianza na wanachama 30 mpaka sasa kina jumla ya wanachama 580

Post a Comment

Previous Post Next Post