WAGOMBEA UDIWANI DODOMA MJINI WASHAURIWA KUTOTEGEMEA FEDHA ZA HALMASHAURI

 


Na Suzana Alex

Prof.mstaafu wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini  David Mwendamaka amewashauri  madiwani watakaochaguliwa kutotegemea fedha zinazotolewa na halmashauri badala yake wakutane na wataalamu wa kuandika miradi ya maendeleo ya kiuchumi

Ushauri huo wa madiwani umetolewa wakati alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa kuwanadi uliofanyika kiwanja cha Hazina Dodoma mjini.

Proff Mwendamaka amewashauri watakapochaguliwa  washirikiane na wataalamu wa kuandika miradi ili waweze kupata fedha kwaajili ya maendeleo ya kwenye kata zao

"Mtakapochaguliwa kuwa madiwani kwenye kata zenu msitegemer sana fedha za halmashauri badala yake mkutane na wataalamu na wadau wa maendeleo ili muweze kuandika miradi kwaajili ya wananchi,



 Naye Mgombea Udiwani kata ya Hazina jimbo la Dodoma Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Lukanus Kayombo akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa  kampeni kata hiyo

Alisema kuwa akichaguliwa atahakikisha anashirikiana na wananchi pamoja na wadau wa maendeleo kuboresha  miundombinu kwani anajua changamoto zilizopo katika kata hiyo.

Amesema atahakikisha mikopo ya asilimia10 inapatikana kwa wazee,kinamama,vijana na watu wenye ulemavu

"Mimi si mgeni hapa najua changamoto za mitaa yote kwasababu nilikua mwenyekiti  wa mtaa,wanakinyambwa tunahitaji mradi wa maji taka, tukae mkao wa kula mradi huo upo njiani wataalamu wameshakuja muda wowote mradi unaanza,"amesema Kayombo

Kwa upande wake Jenesta Malingo mgombea Udiwani mteule kupitia chama hicho Kata ya Zuzu Jimbo la Dodoma amesema atahakikisha anawaondolea kero ya wanafunzi kwa kujenga shule ili kuwapunguzia kutembea mwendo mrefu kufuata elimu

Amesema kwa kushirikiana na wananchi na wadau wa maendelea wataongeza miundombinu mbalimbali kwa kuijenga ikiwemo ya  maji,  zahanati  na vituo vya afya vilivyopo ndani ya Kata.

"Nitasimama imara  katika mabaraza ya madiwani kwa ajili ya kuongelea hali ya uchumi wa wananchi wetu kwa maana ya kwamba ile asilimia 10 ya mikopo inayoenda kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu inawafikia bila upendele"

amesema malingo

Post a Comment

Previous Post Next Post