MIAKA 4 YA DKT.SAMIA TANROADS YAKAMILISHA UJENZI WA BARABARA KILOMETA 1,365.87 KWA KIWANGO CHA LAMI

 


Na Edward Winchislaus.

Mkurugenzi wa mipango ya miundombinu wakala ya barabara Tanzania (TANROADS) Mha.Ephatar Mlavi amesema Serikali ya Awamu ya Sita kuanzia kipindi cha mwaka 2021 hadi Februari 2025 imepata mafanikio makubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara, madaraja na viwanja vya ndege nchini.

Hayo ameyasema leo Februari 17.2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini hapa Dodoma ambapo amesema katika kipindi hicho, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 15,625.55.zimekuwa katika hatua mabalimbali za utekelezaji huku barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 1,365.87 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami na barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 2,031.11 zimeendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.

Amesema barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 2,052.94 na madaraja mawili  zimefanyiwa Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina huku akieleza kuwa Serikali inatafuta fedha za kuzijenga kwa kiwango cha lami. 

"Wakala wa barabara ya Tanzania ( TANROADS) inasimamia ujenzi,ukarabati na matengenezo ya barabara na madaraja kwenye mtandao wa barabara wenye urefu wa jumla ya kilometa 37,435.72.Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa barabara zenye jumla ya kilometa 4,734.43 na madaraja kumi (10) unaendelea. Aidha, miradi ya barabara yenye urefu wa takriban kilometa 5,326.90 na miradi saba (7) ya madaraja ipo katika hatua ya manunuzi kwa ajili ya kufanyiwa Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina  ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara hizo kwa kiwango cha lami.

"Katika kipindi tajwa madaraja makubwa 9 yamekamilika kujengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni Shilingi Bilioni 381.301 kama ifuatavyo: Gerezani (Dsm), Daraja jipya la Tanzanite  (Dsm), Wami (Pwani), Kitengule (Kagera), Kiyegeya (Morogoro), Ruaha (Morogoro), Ruhuhu (Ruvuma), Mpwapwa (Dodoma) na daraja la Msingi singida",amesema.



Pia amesema kuwa Madaraja kumi  ambayo ni pamoja na daraja la Kigongo  Busisi (Magufuli Bridge - Kilometa 3.0), Lower Mpiji lenye kilometa 140, Mbambe lenye kilometa 81, Simiyu lenye kilometa 150,Pangani lenye kilometa 525, Sukuma lenye kilometa 70,Kerema Maziwani lenye kilometa 80,Kibakwe lenye kilometa 30,Mirumba lenye kilometa 60 na Jangwani lenye kilometa 390 ujenzi wake unaendelea kwa gharama ya Shilingi Bilioni 985.802.

"Jumla ya Madaraja makubwa kumi na tisa yako kwenye maandalizi ya kujengwa ambayo ni: Godegode (Dodoma), Ugala (Katavi), Kamshango (Kagera), Bujonde (Mbeya), Bulome (Mbeya), Chakwale (Morogoro), Nguyami (Morogoro), Mkundi (Morogoro), Lower Malagarasi (Kigoma), Mtera (Dodoma), Kyabakoba (Kagera), Mjonga (Morogoro), Doma (Morogoro), Sanga (Songwe), Kalebe (Kagera), Ipyana (Mbeya), Mkondoa (Morogoro), Kilambo (Mtwara) na Chemchem (Singida)",ameeleza.

Katika hatua nyingine Mha.Mlavi amesema kuwa ushiriki wa wakandarasi wazawa katika utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi wa Barabara Kuu na Barabara za Mikoa hairidhishi huku akieleza sababu za ushiriki wao kuwa mdogo ni pamoja na kutoa bei za chini isivyo kawaida katika zabuni,mazingira magumu ya upatikanaji wa mitaji ikilinganishwa na hali ya ushindani na fursa za upendeleo kwa kampuni za wasawa kutozaa matunda yaliyokusudiwa.

"Sababu za ushiriki mdogo wa Makandarasi na Washauri Elekezi Wazawa ni kama ifuatavyo:Kucheleweshwa malipo bila kulipwa riba ya ucheleweshaji,Fursa za upendeleo kwa kampuni za Wazawa kutozaa matunda yaliyokusudiwa,Kutokuwepo mpango mahsusi wa kuendeleza Wazawa,Masharti na vigezo vya zabuni visivyo rafiki kwa makampuni ya Wazawa,Miongozo ya Washirika wa Maendeleo kama WB na AfDB kutotambua upendeleo kwa Wazawa. "Masharti magumu ya kupata dhamana za benki (Bank Guarantees),Kutotengwa kwa miradi mingi kwa ajili ya kukuza uwezo wa Wazawa,Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kutozwa kabla ya malipo kufanyika,Utitiri wa kodi na tozo katika utekelezaji wa miradi ya ujenz na Viwango vikubwa vya kodi ya zuio (Withholding Tax) vinavyotozwa kwenye miradi ya ujenzi",ameeleza Mha.Mlavi.



Aidha amesema kutokana na ushiriki wa wakandarasi wazawa kutoridhisha katika utekelezaji wa muradi mbalimbali TANROADS imechukua hatua kadhaa hadi sasa ili kuongeza ushiriki wa wazawa kama kuendelea kutenga zabuni kwa ajili ya Makandarasi Wazawa katika mpango wa Ununuzi kwa kila mwaka wa fedha,kuendelea Kufuata sheria na kanuni za ununuzi ambazo zimeongeza wigo wa ushiriki wa Makandarasi Wazawa katika zabuni zinazotangazwa kitaifa kufikia TZS 50,000,000.00; pamoja na kuhakikisha ushiriki wa  Wazabuni wandani kwenye zabuni za washauri elekezi kwa kushirikiana na makampuni kutoka nje.

Post a Comment

Previous Post Next Post