BILIONI 234 KUTOLEWA KWA MIKOPO YA ASILIMIA 10

 



Na Edward Winchislaus.


WAZIRI  wa nchi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mhe.Mohamed Mchengerwa amezitaka mamlaka za serikali za mitaa kote nchini kuendelea kuchangia fedha za mapato ya ndani kwaajili ya kuendeleza mikopo ya asilimia 10 kwa wafanyabiashara wadogo wadogo nchni.


Kauli hiyo ameitoa leo Februari 7,2025 katika hafla ya utiaji saini mikataba ya utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kati ya Halmashauri 10 na Benki tatu iliyofanyika jijini hapa Dodoma ambapo amesema fedha inayokusudiwa kuwafikia wananchi  katika awamu ya kwanza ni  Bil. 164 ambapo bilioni 70 ipo kwenye mzunguko na ikirejea jumla ya kiasi cha Bil. 234 kitawafikia wanchi waliyolengwa katika mikopo hiyo.



Mchengerwa amesema benki zilizo idhinishwa kutoa mikopo hiyo katika Halmashauri 10 ni pamoja na Benki ya NMB,CRDB na UCB huku akieleza kuwa Halmashauri nyingine 174 zitaendelea na utowaji wa mikopo kupitia serikali kwa utaratibu uliyoboreshwa.


"Ofisi ya RaisTAMISEMI inasimamia utolewaji wa mikopo kwa  vikundi vya wanawake,vijana na wenye ulemavu inayotokana  na asilimia 10 ya mapato ya ndani yasiyolindwa na Halmashauri kwa mjibu wa sheria ya fedha ya serikali ya mitaa sura 290 kifungu cha 37 (a) utowaji wa mikopo hii ni maelekezo ya Mhe.Rais Dkt.Samia kwaajili ya kuwajali wanawake,vijana na wenye ulemavu ili kuinuwa uchumi wa mtu mmoja moja.


" katika kutekeleza hili mnamo mwezi machi  2023 Mhe.Rais alielekeza mfumo wa utolewaji wa mikopo hii uangaliwe upya ianze kutolewa kwa mfumo wa Benki kwa kuanza na Halmashauri 10,Benki zilizo idhinishwa ni Benki ya CRDB,NMB,na Benki ya uchumi (UCB) ambapo CRDB atasimamia Halimashauri ya Nkasi,Mbulu,Kigoma ujiji,Jiji la Dodoma na Halmashauri ya Jiji la Dar Es Salaam, Benki ya uchumi itasimamia Halmashauri ya Siha,nizielekeze mamlaka za serikali za mitaa kote nchini kuendelea kuchangia fedha za mapato ya ndani kwaajiri ya mikopo hii kwa mjibu wa sheria ya fedha",alisema Mchengerwa.


Aidha Mchengerwa ameelekeza vikundi vyote vinavyopokea mikopo hiyo kuendelea kufanya shughuli za uzalishaji na kurejesha fedha kulingana na mikataba ya mikopo watakayoingia na Halmashauri au Benki hizo huku akiwasisitiza wakuu wa mikoa na Wilaya kuwa suala la usimamizi wa mikopo hiyo ni la kila mmoja wao.



Akitoa salamu za mkoa,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyemule amempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia suluhu hassan kwa kuendelea kuimarisha uchumi jijini Dodoma katika sekta mbalimbali.

Post a Comment

Previous Post Next Post