MIAKA 63 YA UHURU WA TANZANIA BMH INAENDELE KUOKOA MAISHA YA WATOTO WANAOZALIWA KABLA YA WAKATI



Na. Carine Senguji, Dodoma


Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Benjamin Mkapa Prof.  Abel Makubi amewaongoza watumishi wa Benjamin Mkapa kutoa zawadi kwa watoto walio zaliwa kabla ya wakati na wanaohitaji uangalizi maalumu.


"Leo tumekutana kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania kama Rais alivyo agiza kila ofisi ya serikali iadhimishe kwa namna yake,  nasi tumeona ni muhimu kuwakumbuka watoto waliozaliwa kabla ya wakati waliopo hapa hospitalini serikali imewekeza Madaktari na vifaa tiba vya kisasa ambavyo kwa sasa watoto wanaozaliwa kabla ya wakati wanaokolewa hii ni hatua kubwa ya maendeleo katika taifa letu" alisema Prof. Makubi.



Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya watoto Julieth Kabengula amesema Hospitali ya Benjamin mkapa imekuwa ni kimbilio katika kuokoa maisha ya watoto ambao wamezaliwa kabla ya wakati 


"Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kawaida ndani ya mwezi wastani wa watoto waliozaliwa kabla ya wakati 35 hadi 40 wanapokelewa na kuhudumiwa ambapo mpaka sasa tumepokea mtoto mwenye gram ndogo 600 na tulihakikisha anapata matibabu hadi tukamruhusu" amesema Dkt. Julieth


Hata hivyo katika kuadhimisha miaka 63 watumishi wa BMH wametumia kusafisha daraja lililokuwa limezibwa na magogo yaliyo sombwa na mvua. 


"Daraja hili tulilosafisha leo ni kiunganishi pekee kwa watu wote wanaofika Hospitali ya Benjamin Mkapa hivyo kukiwa na shida hapa hatutoweza kuwa salama,  nawashukuru watumishi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kujitokeza kuadhimisha miaka 63 kwa kufanya usafi katika eneo hili" alisema Prof Makubi

Post a Comment

Previous Post Next Post