KIKAO KAZI CHA WAKUU WA IDARA ZA UTAWALA NA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU KATIKA WIZARA NA SEKRETARIETI ZA MIKOA KUFANYIKA JIJINI DODOMA



NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Raisi,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bwana Xavier Daudi ametoa taarifa juu ya maandalizi ya Kikao kazi cha mwaka cha Wakuu wa Idara za utawala na usimamizi wa Rasiliamali watu katika Wizara,Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024 ambayo itafanyika Jijini Dodoma. 



Naibu Katibu Mkuu huyo ameyasema hayo mapema Leo hii Jijini Dodoma Desemba 12,2024 wakati akizungumza na Wanahabari kuelekea kikao hicho.



Na kuongeza kuwa ili kuhakikisha majukumu yanatekelezwa kwa haraka Ofisi imekuwa ikifanya kikao kazi hicho kila mwaka kwa Idara hizo za usimamizi wa rasilimali watu kwa lengo la kubadilishana uzoefu ikiwemo katika masuala mbalimbali  Usiamamizi ya rasilimali watu.



"Ndugu Wanahabari tupo hapa leo tunazungumzia Maandalizi ya Kikao Kazi cha Mwaka cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Idara Zinazojitegemea, Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali kwa mwaka 2024".



 

"Ndugu Wanahabari,pia katika kuhakikisha majukumu yanatekelezwa kwa haraka na kwa ufanisi, Ofisi hii kila mwaka, hufanya Kikao Kazi cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Idara zinazojitegemea, Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali kwa lengo la:-Kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu;Kukumbushana kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma mathalani; matumizi ya mifumo ya kidijitali ya e-Watumishi, e-Uhamisho, e-Utendaji, e-Mrejesho, HR Assessment.Kupeana maelekezo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika utumishi umma kwa kuzingatia Shabaha na vipaumbele vya Taifa".



Naye Bi Felister Shuli ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Umma amesema kuwa Rasilimali watu ni nguzo ya uendeshaji wa rasilimali zingine, hivyo ni muhimu kujengewa uelewa kama ambavyo wamekuwa wakifanya.


SACP Ibrahim Mahumi ambaye ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali watu naye amesema kuwa kwa kukutana huko zipo baadhi ya changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kujadiliwa katika kikao kazi hicho na kuweza kupatiwa ufumbuzi.

 



 Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB) ina majukumu mbalimbali kwa mujibu wa Hati ya Mgawanyo wa Majukumu kwa Mawaziri kama ilivyotangazwa katika Gazeti la Serikali Toleo Na. 619A & 619B la tarehe 30/8/2023. Na Moja ya majukumu hayo ni kusimamia Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma na Utawala wa Utumishi wa Umma.

Post a Comment

Previous Post Next Post