RAIS HUSSEIN MWINYI AMEAHIDI KASI ZAIDI KUKAMILISHA MIRADI

 


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi, amesema  Serikali itaongeza kasi zaidi kukamilisha miradi ya maendeleo kupitia ilani ya utekelezaji ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 kabla ya uchaguzi mkuu. 


Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Ikulu Zanzibar alipokutana na Watendaji wa Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Taifa akiwemo Katibu Mkuu UWT Taifa  Ndg.Suzan Kunambi, Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar  Ndg. Abdi Mahmoud, Naibu Katibu Mkuu Wazazi Zanzibar Ndg.Ali Issa Ali, na Naibu Katibu Mkuu UWT Zanzibar Ndg.Tunu Kondo


Nao Watendaji wa Jumuiya hizo wamempongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa kazi nzuri ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na kuvuka baadhi ya sekta mbalimbali.

Post a Comment

Previous Post Next Post