Idadi ya watu waliofariki baada ya maji ya Bwawa lililopasuka kusomba Kijiji cha Kamuchiri imefikia 42, baada ya miili mingine kuopolewa kutoka kwenye magari 5 ambayo yamekwama kwenye matope.
Mkuu wa Polisi wa Naivasha Stephen Kirui amesema miili ambayo imekwama kwenye matope inatarajiwa kuondolewa na Hospitali ya Mahi Mahiu imejaa baada ya waathiriwa 100 kukimbizwa katika hospitali zote mbili za Mahi Mahiu na Naivasha.


Post a Comment