Na Jasmine shamwepu,Dodoma.
Mkurugenzi wa taasisi ya Tanzanite Fashion na miss utalii Eva Rafael amesema tamasha kubwa la Kitaifa la Tanzanite Fashion week linatarajiwa kufanyika tarehe 4 Mwaka 2024 jijini Dodoma.
Akizungumza na waandshi wa habari leo Dodoma Mkurugenzi huyo amesema kuwa tamasha hilo litaenda kutangaza Utalii wa Madini na Mali asili mbalimbali zilizopo hapa nchini.
"Tunapenda kuwaalika wachimbaji mbalimbali wa Madini, wachimbaji Wanawake na vyama vyao vyote vya Madini, taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi kwenda kushirikiana na sisi katika wiki ya Tanzanite Fashion"Amesema
Aidha amesema kuwa wiki hiyo ni wiki iliyojaa Maudhui mengi,mafundisho pamoja na dhamira nyingi ya kwenda kuigusa jamii na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
" Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuiwezesha sekta ya madini kwa kuchangia asilimia 10 kwenye pato la Taifa ifikapo mwaka 2025 kwa kuondoa changamoto zote zinazowakabili wachimbaji wa madini wadogo wadogo ili kuwezesha shughuli hiyo kuendelea kukua na kukuza uchumi wa nchi ambapo mpaka sasa mchango wa sekta ya madini kwenye pato la nchi umeongezeka kufikia asilimia 9.7"amesema Mkurugenzi huyo
Hata hivyo amesema upekee wa madini ya Tanzanite ambayo mauzo yake hufikia mpaka Dola Milioni hamsini kwa mwaka ndiyo upekee wa shughuli yetu hii ya Tanzanite Fashion week.
Katika hatua nyingine Eva amesema kuwa kwa kutumia Sanaa wanaenda kuleta jukwaa lenye ubunifu wa hali ya juu wa mavazi na mitindo mbalimbali iliyobeba dhima halisi ya madini yetu ya Tanzanite yanayopatikana hapa nchini.
Naye Afisa Utamaduni Wizara ya Utamaduni Sana na Michezo Alice John amempongeza Eva kwa ubunifu huo wa kuandaa tamasha hilo na kusema kuwa anaenda kuieleza na kutumia sanaa kama njia bora ya kufikisha ujumbe
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kanzidata ya madini taasisi ya Jiologia na utafiti wa madini amesema kuwa Madini ya Tanzanite ndo Madini pekee yanayopatikana hapa nchini ndo maana ameyachagua katika wiki ya Tanzanite Fashion week
"Tumeona ni vema kumuunga mkono ili tuweze kuyatangaza madini yetu,tupo na yeye na kama Wizara ya Madini tunasema frusa hii ni bora kwa wachimbaji wadogo Wanawake"Amesema

Post a Comment