Sekta ya kilimo Tanzania imepata pigo kubwa kutokana na kifo cha ghafla cha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Tafiti Za Kilimo ( TARI), Dkt Geofrey Mkamilo.
Marehamu Dkt Mkamilo ambaye aliiongoza taasisi ya TARI kwa miaka kadhaa, amefariki ghafla leo Jumamosi asubuhi, 2 Machi, 2024 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma baadaya kulazwa kwa muda mfupi.
Pmoja na mambo mengine, wakati wa enzi ya uhai wake, marehemu Dkt Mkamilo zake atakumbukwa daima kwa nafasi yake ya juu, pamoja na moyo wa uzalendo katika kuwaongoza wafanyakazi wengine na wataalamu wa kilimo kufanya kazi usiku na kucha katika jitihada za jumla za utafiti, uvumbuzi na uzalishia wa mbegu bora za mazao mbalimbali, hatua ambayo imechochea kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo nchini Tanzania.

Post a Comment