MAYELE AMPONGEZA FEI TOTO

 


Mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC ambae kwa sasa anaekipiga kwenye klabu ya Pyramid Misri, Fiston Mayele amempongeza Mchezaji wa Azam FC ambae nae amewahi kukipiga Yanga Feisal Salum baada ya kufunga goli la ushindi wa 2-1 kwenye mchezo dhidi ya waajiri wake wa zamani (Yanga SC).



Mayele amempongeza Feisal kupitia kwenye post ambayo Feisal aliipost kwenye ukurasa wake inayoonyesha goli alilofunga kwenye mchezo huo na MAYELE aliacha comment fupi "Hongera bro".



Huu unakuwa mchezo wa tatu kwa Feisal kukutana na Yanga toka ajiunge na Azam FC na linakuwa goli lake la kwanza kuiwamba Yanga toka aondoke kwenye viunga vya twiga na Jangwani

Post a Comment

Previous Post Next Post