Walimu Ni Chumvi Katika Elimu -Askofu

 

Askofu wa kanisa la Angilikana Dayosisi ya Mount Kilimanjaro Dokta Stanley Hotay ameeleza kuwa hakuna nchi yoyote duniaani iliyoendelea pasipo elimu na walimu ni kama chumvi ya dunia Mt.5:13

Askofu Stanley Hotay ameeleza hayo leo februari 8,2024 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha mwaka kwa wamiliki wa shule za kanisa nchini

Aidha amesema kuwa wanasiasa washughulike na majengo na sio elimu suala la elimu liachiwe na wanataaluma,pia kinachojadiliwa katika elimu ni ubora na sio wingi wa wanafunzi

Ameongeza kuwa waanzilishi wa elimu nchini ni makanisa toka enzi za ukoloni na kubainisha kuwa shule za kanisa zimezalisha viongozi wengi

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Kikristo ya huduma za jamii (CSSC) Peter Maduki amewapongeza wote viongozi na wafanyakazi wa shule za kanisa kwa kazi nzuri wanayofanya ya kuwapokea na kuwalea watoto kwa malezi na elimu bora

Pia amesema inabidi waendelee kutoa huduma endelevu ya elimu,kuimarisha uongozi wa shule na kufata utaratibu uliowekwa na serikali

Naye Joshua Moshi mshauri wa huduma za elimu kutoka CSSC ameeleza kuwa wamekutana Dodoma kwa ajili ya kujadili ni namna gani wanaweza kutekeleza mtaala mpya wa elimu ulioanza kutumika mwaka huu kwa elimu ya msingi na sekondari

Post a Comment

Previous Post Next Post