Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa ambaye pia ni Mlezi wa CCM Mikoa ya Kusini na Kaskazini Unguja Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Mikoa hiyo katika Ukumbi wa Ofisi ndogo ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizopo Tunguu, Zanzibar leo tarehe 15 Januari, 2024.
Pamoja na mambo mengine, Viongozi hao wamejadili kuhusu maandalizi ya ziara za Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mikoa ya Unguja inayotarajiwa kufanyika Januari 17 na 18, 2024.


Post a Comment