Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema ni wakati
umefika kwa watunga sera barani Afrika kutambua umuhimu wa kilimo na wakulima
ili kuweza kutumia vema fursa ya ardhi ya Afrika kujiletea maendeleo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumzawakatiwamjadalawa“kutengenezafursakatikaardhiya
Afrika”uliyofanyika katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) unaofanyika
Davos nchini Uswisi.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akishiriki mjadala unaohusu
“kutengeneza fursa katika ardhi ya Afrika” uliyofanyika katika Mkutano wa
Jukwaa la Uchumi Duniani unaofanyika Davos nchini Uswisi. Amesema ni muhimu
watunga sera wa Afrika kutambua umuhimu wa wakulima kwa kuwa ndiyo wanaohakikisha
usalama wa chakula, kuongeza fedha za kigeni pamoja na kuongeza upatikanaji wa
mapato ya serikali.
Amesema ni muhimu kuondoa sera zisizo rafiki ili kuwasaidia wakulima
kufikia masoko kirahisi na kupata haki ya kile wanachozalisha. Pia amesema
mikopo kwa wakulima kwa riba nafuu itasaidia ukuaji wa kilimo barani Afrika.
Makamu wa Rais amesema Tanzania imeendelea na jitihada za kuboresha
sekta ya kilimo kwa kuongeza bajeti ya kilimo mara tatu zaidi, kuongeza huduma
za ugani ikiwemo kutoa vitendea kazi kwa maafisa ugani na kufanya ufuatiliaji
wa wakulima wa mara kwa mara. Aidha amesema serikali imeendelea kuweka mkazo
kwa wakulima kubadilisha uzoefu wao kwa wao pamoja na kujenga miundombinu ya
umwagiliaji ikiwemo visima vya maji kwa wakulima wadogo. Pia Tanzania
inashirikiana na wadau katika upimaji wa afya udongo, utoaji mbolea kulingana
na maeneo husika ya kilimo pamoja na kukaribisha uwekezaji katika ujenzi wa
viwanda vya uzalishaji mbolea.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumzawakatiwamjadalawa“kutengenezafursakatikaardhiya
Afrika”uliyofanyika katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) unaofanyika
Davos nchini Uswisi.
Halikadhalika Makamu wa Rais amesema jitihada zinapaswa kufanyika barani
Afrika katika kupanga matumizi ya ardhi, kupima afya ya udongo ili kuweza
kutambua aina ya mazao na mbolea itakayofaa katika maeneo fulani ya kilimo na
hivyo kuongeza uzalishaji.
Makamu wa Rais amewakaribisha wawekezaji, sekta binafsi na wadau
kushirikiana na Tanzania katika sekta ya kilimo ikiwemo ujenzi wa maghala ya
uhifadhi wa mazao.


Post a Comment