Wanafunzi Wasiosikia Asilimia 59 Wanashindwa Kuandika

  Wanafunzi wa Sekondari wenye ulemavu wa usikivu (Viziwi) Asilimia 59 ya bado wanashindwa kuandika kutokana na kutojengewa msingi mzuri tangu wakiwa  shule za msingi


Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Tabora Aaron Vedasto kwenye warsha ya wadau wa sekta ya elimu iliyofanyika katika ukumbi wa JB Mkoani Tabora



Alisema kwamba utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu Cha AMUCTA mkoani hapa umeonyesha wanafunzi ni 404 wenye tatizo hilo  ambao waliopimwa 96 hawakuweza kuandika na 86 ni uwezo wa chini ,walipimwa uelewa wa kujua kuandika au kuongea kwa lugha ya alama.


Afisa Elimu huyo alisema kwamba Wakati nchi ya Tanzania ikiendelea kutekeleza mikakati ya sekta ya elimu jumuishi unaolenga kuwaweka pamoja wananfunzi wenye mahitaji maalum  ili kuleta usawa na kuondoa unyanyapaa wengi wao waliachwa nyuma


Afisa huyo amekipongeza Chuo Kikuu Cha AMUCTA kwa kufanya utafiti kwa wanafunzi hao kutoka katika shule za sekondari  ambapo Serikali  imekua ikitekeleza mikakati ya elimu jumuishi unaowaweka pamoja wanafunzi wenye ulemavu na wale wasio na ulemavu likiwa  lengo ni kuleta usawa na kuondoa unyanyapaa.


Alisema serikali kwa kuliona tatizo hilo Chuo Kikuu Cha Amucta Mkoani Tabora  kimelazimika kufanya utafiti ili kubaini kama mpango huo wa elimu jumuishi  unatekelezwa ipasavyo ambapo takribani wanafunzi  404 walipimwa uelewa wa kujua kuandika au kuongea kwa lugha ya alama.


"Nakiri bado changamoto ni kubwa kwenye elimu jumuishi lakini serikali yetu itaendelea kupokea maoni na  kuyafanyia kazi na kuona namna gani itaweza kutusaidia juu ya elimu   ili kuboresha sekta hiyo muhimu hapa nchini"  alisema Aaron   


Akisoma Taarifa ya utafiti katika kikao cha kitaaluma Padri Dkt Apolinary Ndasi kutoka Chuo Kikuu Cha AMUCTA mkoani Tabora alisema kwamba wajibu wao ni kufundisha , kufanya utafiti na kutoa huduma kwa jamii.



Alisema kwamba chuo hicho kiliweka mikakati baada ya kuona mianya inayojitokeza kwenye elimu ya wanafunzi wasiosikia wengine kuacha shule na uzoefu wa walimu katika ufundisha kuwa ni tatizo kubwa .


 Aidha Dkt Ndasi alisema kwa kuwa ni wajibu wao kutoa huduma kutalenga uboreshaji elimu kwa kutoa maarifa na kuwaweka walimu wenye ujuzi ambao wataweza wafundisha wanafunzi hao.


Hata hivyo Chuo Kikuu Cha Amucta Walilenga kuwaendeleza walimu wakuu na waratibu elimu kata kuwaongezea ujuzi na usimamizi wa uwendeshaji katika shule za wanafunzi wasiosikia.


Dkt Padri Ndasi alibainisha kwamba baada ya kuwafanya tathimini kwa wanafunzi  96 waliweza kuandika Sawa na asilimia 56 na wenginge waliweza kuandika kwa kutumia lugha ya alama ,lakini kwa kuandika maandishi walikuwa wanashindwa.


Changamoto nyingine ni walimu kushindwa kufundisha lugha ya alama kwa  wanafunzi wasiosikia kwa sababu hawakupata mafunzo ya ufundishaji.


Nao baadhi ya wadau wa elimu kata ya mwinyi mkoani hapa Mwalimu Masumbuko Abeli alitoa ushauri kwa maafisa elimu wote wakafanye upembuzi yakinifu kwa walimu wa kufundisha wanafunzi wenye uhitaji maalum kama wana ustawi ya kufundisha.




Wadau hao walikiomba chuo hicho kufanya semina za mara kwa mara kwa walimu ili kuweza kuboresha taaluma katika sekta ya elimu kwa wanafunzi wenye matatizo ya kutosikia ili waweze kuendelea na masomo katika shule mbalimbali nchini .

 

Nae Mthibiti Mkuu wa Ubora wa shule   Manispaa ya  Tabora, Florencia Vincent aliishukuru serikali kwa kuwaletea walimu vifaa mbalimbali  na iendelee kuongeza walimu wenye ujuzi wa elimu na taaluma ,kwani kwa sasa hawatoshi kutokana na idadi iliyopo.

Post a Comment

Previous Post Next Post