Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limeendelea kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva na abiria katika stendi ya Nyagezi ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani.
Akizungumza na madereva pamoja na abiria wakati wa elimu hiyo Novemba 23, 2023, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Wilbroad Mutafungwa amewataka madereva kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za barabarani huku akionya watakaokiuka kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
mbali na hilo pia kamanda Mutafungwa ameonya wahalifu wenye nia ya kuingia mkoani humo kipindi cha sikukuu za mwisho wa Mwaka kuwa hawatoingia na kutoka wakiwa salama kwani tayari Operesheni kali, misako na doria zimeimarishwa kila kona kuhakikisha hakuna uhalifu utakaofanyika.
Aidha, amewatakia abiria na madereva hao safari njema huku akiwasisitiza kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa Polisi pale watakapoona changamoto yoyote njiani.
Kwa upande wake mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoani hapa Mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP) Sunday Ibrahim mbali na kutoa elimu pia ameahidi kusimamia sheria za Usalama barabarani.



Post a Comment