Mashaka Kibaya,Moshi.
Kampuni ya kizalendo Zara Tanzania Adventure iliyopo wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro kupitia Zara Charity imewekeza kwenye Sekta ya elimu na kuweza kuokoa watoto wengi wanaotoka Jamii za wafugaji waliokuwa wakiishi mazingira magumu na hivyo kuwaepusha kwenye uwezekano wa kutumbukia kwenye makundi hatarishi.
Watoto wanaopatiwa elimu na Moshi Kids Centre wakifurahia Drone iliyokuwa ikichukua picha.
ambayo ameshinda kwa miaka miwili mfululizo.
Miundombinu hiyo ya elimu imejengwa Moshi ambapo kuna kituo cha elimu cha Moshi Kids Centre kinachohudumia Watoto wadogo wakifanyiwa maandalizi ya kwenda kujiunga Shule za Msingi,eneo ambalo limefanikiwa kuwa na mazingira rafiki na yenye usalama.
Eneo jingine ambalo Zara Tanzania Adventure imefanya wekeza kwenye Elimu ni huko Karatu kulikoweza kujengwa Shule mbili zenye mchango mkubwa kwa Watoto wa Jamii za Wafugaji huku wadau wengine wakinufaika kwa uwepo miradi ya afya.
Peace Festo Mugele ni Msimamizi wa Kituo cha Moshi Kids Centre kilichoasisiwa na Mkurugenzi wa Zara Tanzania Adventure, Zainab Ansell, kupitia Zara Charity ambapo leo Kituo hicho kimekuwa mkombozi mkubwa kwa Watoto waliopo Mjini Moshi.
Mugele anasema,kituo hicho kilichopo eneo la Pasua Kata ya Kaloleni Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kinachukua Watoto wanaotoka kwenye mazingira makumu kuanzia umri wa miaka miatatu hadi kufikia mitano.
Kwa mujibu wa Mugele, Moshi Kids Centre ilianza rasmi kazi zake mnamo mwezi Agosti Mwaka jana ikiwa moja ya miradi ya Zara Charity ambapo watoto wanaojiunga hupatikana baada ya kutembelewa ili kuweza kutambuliwa baada ya kutembelewa ili kuweza kutambuliwa.
"Tumekuwa tukishirikiana na Mabalozi na Wenyeviti katika kuwabaini watoto wenye mahitaji na tunawasaidia bure,tunawapatia elimu hatua ambayo inawaepusha kuzurura ovyo mitaani"anasema Peace Festo Mugele.
Msimamizi huyo wa Moshi Kids Centre anasema kuwa,walianza wakiwa na darasa moja lenye watoto 25 na mwaka huu wameongeza jingine likiwa na idadi kama hiyo ya watoto huku uhitaji ukionekana kwamba bado ni mkubwa.
Kituo hicho cha elimu ya watoto yaani Moshi Kids Centre kina Walimu wawili, mpishi mmoja,mlinzi mmoja,kijana anaye shughulikia Usafi wa mazingira mmoja na hivyo kufanya Wafanyakazi kufikia Sita pamoja na Bi.Mugele.
Hata hivyo Mugele anatanabaisha kuwa bado kuna mahitaji ya darasa jingine moja huku akielezea shukrani zake kwa Bi Zainab Ansell aliyetoa Kiwanja chake sanjari na kuhusika ujenzi kituo hicho.
Licha ya kwamba Zara Charity imekuwa ikiendelea kuwahudumia Watoto kwa Chakula,elimu na mahitaji mengine ya msingi kupitia kituo chake cha Moshi Kids Centre, bado kuna haja ya wadau wanaowiwa kujitokeza ili kutoa misaada.
"Huwa tunawalea watoto hawa kwa kuwalea kwenye mazingira haya rafiki kama unavyoona,tunawapa elimu,chakula kuanzia uji unaoatikana ingawa tunaomba wadau wenye moyo watusaidie"anasema Bi Mugele.
Msimamizi huyo wa kituo cha elimu Moshi Kids Centre anaendelea kumshukuru Mkurugenzi wa Zara Tanzania Adventure, Zainab Ansell ambaye amekuwa mstari wa mbele kushiriki kuwapeleka wageni wanaotaka kutoa misaada kwa watoto kituoni hapo.
Huu unaonekana kuwa mchango mkubwa wa Zara Tanzania Adventure ambapo kupitia Sekta ya Utalii imeanzisha miradi mbalimbali ambayo leo inaonekana kuwa msaada kwa jamii.
Zainab Ansell maarufu kama Mama Zara anasema kwamba,kwa kila kinachopokelewa kutoka kwa wageni kimekuwa kikiratibiwa na kuna muda ukifika taarifa huwekwa hadharani.
Kwa nini Zainab Ansell amekuwa akifahamika sana kwa jina maarufu la Mama Zara? Hii ni kwa sababu ya mchango wake anaoutoa kwa shughuli za Kijamii amekuwa akijitoa kwa moyo wake wa huruma kama ilivyo tabia za Wanawake wengi miongoni mwa jamii.
Mchango wa Mama Zara kwenye shughuli za Kijamii umekuwa ukionekana maeneo mbalimbali huku akifanikiwa kuajiri idadi kubwa ya Watanzania sanjari na kuendesha Program za kujitolea kwa Watembeza wageni 'Tour Guide' ambao Zara Tanzania Adventure imekuwa ikiwaongezea uwezo kitaaluma.
Miongoni mwa waongoza wageni hao,wapo walioajiriwa na Kampuni ya Zara Tanzania Adventure huku wengine wakipata ajira kwenye maeneo mengine baada ya kupatiwa mafunzo stahiki.
Akiwa Mwanamke anayeweza kuonekana wa pekee anayeendelea kufanya vyema kwenye Sekta ya Utalii,Zainab Ansell anawasihi Wanawake wengine wa kitanzania kutokata tamara na kurudi nyuma pindi wanapokusudia kuanzisha biashara.
Anasema kwamba,katika uanIshaji wa kila jambo kuna changamoto nyingi akitaja kuanguka ambapo alisema mambo ya aina hiyo vyema yakachukuliwa kama funzo la kuweza kusaidia kupiga hatua kimaendeleo.
Mohamed Abdallah maarufu kwa jina la Madili Simba ni mtembeza wageni Mkongwe 'Tour Guide' ambaye anamwelezea Mama Zara kuwa mwenye huruma na upendo kwa wafanyakazi wake na ndio sababu wengi wamemuona kuwa sawa na Mama yao.
Abdallah anasema kwamba, Mama Zara amekuwa mlezi wao anayepaswa kuungwa mkono ili kuendelea kuisaidia sehemu kubwa ya jamii ya Watanzania.



Post a Comment