TMA Yatoa Tahadhari Ya Mvua Siku Nne Mfululizo Katika Mikoa Hii

 DAE ES SALAAM

Mamlaka ya hali ya hewa tanzania [TMA] imetoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa kuanzia leo Jumatano Novemba 22  Hadi Novemba 25 ambapo huenda zitasababisha vifo ikiwa Tahadhali hazitachukuliwa.

TMA imesema mvua hizo zinatarajia kunyesha katika Mikoa ya  dar es salaam,morogoro,pwani,lindi,mtwara,tanga na visiwa vya Mafia, unguja na pemba



Taarifa ya mamlaka hiyo imetolewa jumanne novemba 21,2023 katika mitandao yao ya kijamii inaeleza athali zinazoweza kujitokeza ni pamoja na baadi ya Barabara kutopitika kutokana na mafuriko, pamoja na vifo hivyo wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari mapema.

pia TMA imetoa maangalizo kuwa mvua hizo kuendelea ijumaa hadi jumamosi kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Dar es salaam, tanga, pwani, mafia 

Agosti 26,2023 TMA ilitoa taarifa  ya uwezekano wa kuwapo kwa mvua kubwa za El-Nino ambazo huenda zikasababisha vifo, magonjwa ya mlipuko na uharibifu wa miundombinu kuanzia Oktoba hadi Desemba 2023.

TMA ilisema mvua hizo zitasababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi, upotevu wa mali na madhara kwa binadamu na mazingira.

Kutokana na hali hiyo, TMA ilizishauri sekta na taasisi mbalimbali, zikiwamo za kilimo, mifugo, uvuvi, utalii, wanyamapori, uchukuzi, mamlaka za miji, nishati, maji na madini, sekta binafsi, Wizara ya Afya na menejimenti za maafa kuchukua hatua mapema kabla ya kuanza kwa mvua hizo.

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Ladislaus Chang’a alisema utabili unaonyesha mvua zitakuwa juu ya wastani, huku akishauri sekta mbalimbali zijiandae kukabiliana na majanga.

“Mvua za vuli zinatarajiwa kuanza Oktoba mwaka huu katika maeneo mengi nchini na zitakuwa za wastani na wastani wa juu itanyesha Pwani ya kaskazini na ukanda wa Ziwa Victoria,”alisema Dk Chang’a.

Maeneo mengine ni magharibi inayojumuisha mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara pamoja na kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma (wilaya za Kakonko na Kibondo), ukanda wa pwani ya kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Pwani, Dar es Salaam, Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba.

“Hivyo, Idara ya menejimenti ya maafa nchini inashauriwa kuendelea kuratibu utekelezaji wa mipango itakayosaidia kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza,” alisema Dk Chang’a.

Post a Comment

Previous Post Next Post