Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amefungua soko la mbagala Zakhem lenye thamani ya shilingiBilioni 2.48 uku akiwataka watendaji kuhakikisha wanasimamia mapato kwa ufanisi jambo ambalo litasaidia kuleta tija kwa kuendelea kufanya maboresho katika maeneo ya kufanyia biashara.
Akizungumza jijini dae es salaam katikahalfa ya ufunguzi wa soko hilo RC Chalamila Amesema kuwa mtendaji yeyote atakayebainika analeta ubabaishaji atachukuliwa hatua za kisheria huku akiwataka wafanyabiashara wote kuanza kufanya biashara ndani ya mwezi mmoja katika soko hilo.
Nayr Meneja wa wakala wa Barabara mjini na vijijini [TARURA] Wilaya ya Temeke Mhadisi PAUL MHERE amesema kuwa lengpo la mradi ni kuboresha miundombinu ya soko, kuongeza mapato na idadi ya wafanyabiashara kutoka 208 hadi 500.

Post a Comment