Jiji La Lawataka Machinga Kufanya Biashara Zao Kwenye Maeneo Waliotengwa Na Siyo Barabarani naMitaani.

 Na Peter Mkwavila DODOMA

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imesema kuwa litaendelea kuwaondoa wamachinga wanaojenga vibanda vya kufanyia biashara zao katika maeneo yasiyo ruhusiwa ikiwemo barabara zinazotumiwa na waenda kwa miguu na pembezoni mwa majengo ya serikali kwa kuwa zoezi hilo ni la kudumu na siyo la muda mfupi.


Kauli hiyo imesemwa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma John Kayombo alipokuwa akijibu majibu kutoka kwa Madiwani wa kata kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha robo mwaka kilichofanyika Jijini Dodoma.

Madiwani hao walitaka kujua mkakati uliopo wa Jiji juu ya kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo machinga ambao wameanza kurudi mitaani kufanya biashara na wengine kujenga mabanda kwenye maeneo ya majengo ya taasisi na wale wanaopanga barabara za watembea kwa miguu badala ya maeneo walikopangiwa likiwemo soko la Machinga na Ndugai.

Kayombo alisema kuwa mkakati wa Jiji ni kuhakikisha hakuna wafanyabiashara wadogo wadogo machinga watakaoruhusiwa kufanya biashara zao kwenye maeneo ambayo hayaruhusiwi na kama wameanza kurudi wataondolewa kwa kuwa zoezi hili ni la kudumu na siyo la kipindi kifupi.

"Niwahakikishie Madiwani wa Jiji kuwa hakuna kibanda chochote kilichopo kwenye maeneo ya taasisi za kiserikali,nyumba za watu binafsi kwenye barabara za waenda kwa miguu watakaoachwa,lazima watabomolewa vibanda vyao hivyo na kuondolewa na kuchukuliwa hatua za sheria za zilizojiwekea na Jiji ikiwemo faini au kufungwa jela"alisema

Kayombo alisema kuwa kila kata kuna masoko yake hivyo sione sababu ya wafanyabiashara hao ndogondogo machinga kurudi mitaani na kujipangia kufanya biashara maeneo ambayo hayaruhusiwi wakati  wakifaya hivyo wanafahamu wanakiuka sheria zilizojiwekea na Jiji.

Awali wakichangia kwenye kikao hicho cha baraza la Madiwaji cha robo mwaka kilichofanyika Jijini hapa,Diwani wa Kata ya Kikuyu kusini Anselem Kutika,aisema kuwa wamachinga tayari wameanza kuzangaa mitaani na kupanga biashara maeneo yaliyozuiliwa kufanya biashara wakati kuna wamepangiwa 

Kutika alisema kuwa Jiji linatakiwa kufanya maamuzi yake ambayo hayatajirudia kama hili la wafanyabiashara ndogo ndogo hao machinga kuanza kurudi tena kwenye maeneo ambayo walishaondolewa baada ya kutengewa sehemu zingine zikiwemo kwenye masoko yaliyopo katika kata zetu.

Naye diwani wa viti maalumu Joyce George amewaomba madiwani kushirikiana na Jiji katika kutoa elimu kwa wafanyabiashara hao ili kuwaepusha na hasara wanazozipata za kubombolewa na kunyanganywa bidhaa zao pale wanapokutwa kwenye maeneo yasiyoruhusiwa.
MWISHO  

Post a Comment

Previous Post Next Post