"Sweden imekuwa ni moja ya nchini muhimu
inayochangia kwa kiasi kikubwa kwenye miradi ya Nishati hususani umeme imechangia
shilingi bilioni 142 kwenye miradi ya ujazilizi kwenye vitongoji 1328 na Vijiji
takriban 151 imechangia shilingi bilioni 52’’ . Amesema Waziri Biteko
Pia amesema kuwa kwa sasa wanajipanga kuongeza nguvu kwenye uwekezaji sekta ya nishati na kuwataka wadau wa sekta ya hiyo kuitumia vizuri fursa ya mikopo na misaada ya wadau wa maendeleo kama Sweden ili kuendelea kuleta maendeleo kwa wananchi.
Hata hivyo Waziri Biteko ameipongeza kampuni ya Scania kwa kuja na Teknolojia mpya ya kutumia taka ngumu kuzigeuza kuwa nishati ya kuendeshea magari na mitambo, hivyo taka zinazozalishwa hapa nchini zitageuzwa kuwa nishati ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kwa upande wake Balozi wa Sweden Charlotta Ozaki amesema kuwa uhusiano wa ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden uliasisiwa na Rais wa awamu ya kwanza Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Waziri Mkuu wa Sweden kwa wakati huo na kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano hadi leo.
‘’tangu ushirikiano huo uanze mwaka1963 hadi Leo 2023 tayari Sweden imetoa misaada ya takriban dola bilioni 8 kusaidia sekta ya nishati ikiwemo ujenzi wa miundo mbinu ya umeme na miradi ya umeme vijijini’’


.jpg)

Post a Comment