Msigwa Amkabidhi Ofisi Mkurugenzi Mpya Wa Idara Ya Habari Maelezo


 
Na Anna George DODOMA.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa  Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa   amekabidhi Ofisi kwa mrithi wake  Mobhare Matinyi huku akieleza  kuwa anaondoka akiwa na jambo linalomsumbua la  hali ya vyombo vya habari na uchumi wa waandishi wa habari.


Msigwa ameyasema hayo leo Oktoba 6,2023 jijini Dodoma wakati wa hafla ya makabidhiano ya  ofisi ya Idara ya Habari Maelezo kwa Matinyi ambaye kabla ya kuteuliwa na Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke.

Msigwa ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa  na Michezo amesema " jambo ambalo nilitamani kulifanyia kazi ni kuhakikisha uchumi wa vyombo vya habari na waandishi wa habari unaimarika na nimeondoka wakati  bado haujaimarika na kupelekea waandishi wengi kufanya kazi hiyo kwa kujitolea badala ya kupata ajira zinazoweza kuwapatia kipato,"




Kwa upande mwingine Msigwa ameahidi kutekeleza wajibu aliotumwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhakikisha Wizara hiyo  inaleta furaha kwa watanzani  kiuchumi na kiafya.

Amewashukuru waandishi wa Habari na kutaka ushirikiano huo uendelee kwa msemaji mpya huyo aliye

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa habari maelezo ndug.Matime ameahidi  kufanya kazi kwa juhudi zote kwa kushirikiana na Taasisi zote ili kutimiza malengo ya Mhe. Rais za kutangaza kazi zinazofanyika




Matime ameahidi kushirikiana na Waandishi wa Habari kwa kuhabarisha umma juu ya Mambo yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita.

Pia emeongeza kuwa waandishi wa habari wanapaswa kutumia vyema kalamu zao kwenda kwa wananchi kuandika mazuri yanayofanywa na Rais Samia katika kuwaleta maendeleo.




Post a Comment

Previous Post Next Post