Kurejea Kwa Gulio La Nyahanga Kuzingatie Suala La Mazingira

 WADAU wa Mazingira katika Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga wametoa ushauri kwa Afisa mazingira wa manispaa hiyo kuhamasisha suala la usafi wa mazingira katika gulio hilo lililorejeshwa siku ya jumamosi badala ya jumatatu kwa madai ni siku nzuri ambayo wanafunzi wa shule ya msingi Nyahanga hawapo.



Wakizungumza kwa sharti la kutoandikwa majina yao wadau hao wamesema kuwa soko ambalo lilikuwa ni gulio la kila jumatatu na likafungwa na mkurugenzi wa Manispaa hiyo Anderson Msumba kutokana na kuwa eneo hilo ni bavazoni lakini linapakana na shule sasa limerejeshwa siku ya jumamosi.

Aidha wamesema kuwa pamoja na kurejeshwa siku ya jumamosi hali ya mazingira katika eneo hilo ni hatarishi ukilinganisha choo kinakuwa kimefungwa wakati wajasiriamali wanaendele na biashara.

“Choo kimefungwa na kufuri, wafanyabiashara hao wanajisaidia wapi badala yake si watajisaidia vichakani na kufanya uchafuzi wa mazingira lakini pia kwenye eneo hilo watu wanaolewa pombe wamegeuza ni eneo la kupunzikia na kulala hivyo tunaomba afisa anayehusika na mazingira afanye ziara hapo hasa siku za jumamosi za gulio hilo,” alisema mmoja wa wadau wa mazingira bila kutaja jina.

Aidha wamehoji kuwa kama mkurugenzi hapo awali alichukua hatua ya kulifunga gulio hilo na kuwatangazia inakuaje tena badala ya jumatatu imekuwa jumamosi tena.

Hata hivyo pamoja na mambo mengine nao wajasiriamali walioongea na Sema Swahili wameeleza kuwa siku ya jumamosi ingefutwa na kurejeshwa siku ya jumatatu kwakuwa siku hiyo kunakuwa na mgongano wa magulio mengi sehemu mbalimbali wilayani Kahama ambapo asilimia kubwa wafanyabiashara wengi wanakwenda kwenye magulio makubwa jambo ambalo hata wateja hawawezi kupata.

“Kwa kweli licha ya kumshukuru mkurugenzi kwa kuruhusu biashara ziendelee kwenye eneo hili siku za jumamosi lakini sisi tunaomba hili gulio lirudishwe siku ya jumatatu kwani leo jumamosi wengi wamekwenda kwenye minada mikubwa huko maeneo mengine kwamana hiyo hapa tupotupo tu hata wateja siyo kama mwanzo,” alisema.

Naye mdau mwingine wa maendeleo kwa sharti la kutoandikwa jina lake gazetini alisema kipindi cha soko lipo kila jumatatu wajasiriamali waliuza mpaka laki tatu nne kwa siku lakini leo siku ya jumamosi bado hawajaona kitu.



Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nyahanga Ikongoli Ikongoli katika mahojiano na mwandishi wa habari hizi alisema Gulio limerejeshwa siku ya jumamosi ili wafanyabiashara wapate chochote badala ya kukatazwa jumla lakini pia kuisha siku ya jumatatu ambako ni siku za shule na wanafunzi hao wanaweza kuwa wanajificha katika eneo hilo na kutohudhulia masomo.

Alisema kuwa kule walikokuwa mwanzo hawafanyi biashara zao kwa ufanisi lakini kwa hapa ni papana na wanaweza kuwa na wateja wengi zaidi kulingana na kwamba ni barabarani ambako kuna makazi mengi ya wananchi wanaokuja kuwahudumia.



Kuhusu kufunga kufuli aliwataka uongozi wa gulio hilo wafungue mara moja siyo mpaka mkurugenzi apige kelele ama atishie kuwafungia tena ndiyo wawe makini na kuahidi kila siku ya gulio hilo atahakikisha kuwa anafanya ziara ya kufika hapo ili kujiridhisha kama huduma zipo sawa kwa wafanyabiashara hao.

Post a Comment

Previous Post Next Post