Eng.Hango Aonya Matapeli wanaotumia jina la Maofisa Madini kutapeli wachimbaji wadogo.

 


N aPaul Kayanda,Kahama

 

AFISA Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini Kahama Mhandisi Jeremiah Hango amewataka Matapeli kutafuta kazi nyingine za kuliko kutumia jina la Maafisa Madini kutapeli wachimbaji Wadogo na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

 


Akizungumza na waandishi wa Habari leo Ofisini kwake,Eng Hango amesema kuwa katika maeneo mbalimbali kumekuwa na migogoro midogomidogo lakini amebainisha kuwa chanzo cha migogoro hiyo ni baadhi ya Matapeli kuamua kuwatapeli wachimbaji huku wakitumia jina la Maafisa Madini.

 

Kufuatia kushamiri kwa kasi ya utapeli huo,Eng Hango amefafanua kwamba wachimbaji lazima waelewe kuwa katika tasnia ya uchimbaji Madini kuna Wizara mbili zinazohusika, na kila Wizara ina majukumu yake ya kiutendaji.

 

Afi


sa huyo wa Madini amezitaja Wizara hizo kuwa ni pamoja na Wizara ya Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi ambayo kazi yake ni kushughulika na migogoro ya Ardhi pekee huku Wizara ya Madini ikishughulikia masuala ya Leseni pamoja na usimamizi wa Maduhuli ya Serikali.

 

Hango alisema kuchanganya majukumu ya Wizara ya Ardhi na kupandikiza migogoro kwa Tume ya Madini siyo jambo jema bali wachimbaji wafuate utaratibu kupitia Ofisi husika ili iweze kutafuta ufumbuzi wa changamoto zao.

 

"Kama suala linahusu Ardhi sisi upande wa Tume ya Madini hatuhusiki kabisa sisi wajibu wetu ni kusimamia wachimbaji wachimbe kwa kufuata Sheria na taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Madini kwa hiyo niwaombe sana wachimbaji waache kulalamika kwani Ofisi hii ni yao nawakaribisha ili tushirikiane kuhakaikisha hawapati changamoto yoyote "alisema Eng Hango.

 

Aidha kuanzia sasa Ofisi ya Tume ya Madini Kahama imeelekeza kuwa,Migogo ya Ardhi ikatatuliwe na wahusika badala ya kukaa wakiwanyooshea  vidole watendaji wa Tume hasa  katika eneo ambalo si sehemu ya majukumu yao,alisisitiza.

 

Kufuatia mgogoro uliopo baina ya Wamiliki wa Shamba na mmiliki wa Leseni Kembo and Partners iliyoko Mwime Kata ya Zongomela Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Kimadini wa Kahama Eng Jeremia Hango ameelekeza kuwa mgogoro huo unapaswa kutatuliwa na Baraza la Ardhi la Wilaya.

 

Eng Hango pia ameelekeza kuwa shughuli za uchimbaji wa Madini ziendelee katika eneo hilo kwani wachimbaji hawahusiki na mgogoro huo na kwamba mmiliki wa Leseni hataruhusiwa kuchukua Mapato yoyote na yatatunzwa na Serikali mpaka hapo mgogoro huo utakapotatuliwa.

 

“Kwa mana hiyo Ofisi ya Tume ya Madini Kahama inamwelekeza Kembo kuwasilisha Nyaraka zinazohusu Shamba  kwa mujibu wa matakwa ya barua yenye kumbu Na. HA.366/457/278/08 ya tarehe 03/10/2023 kama Sheria ya Madini kifungu Na.95(a) (1)ya Sheria ya Madini Sura Na.123.

 

Hata hivyo Afisa Madini huyo ameonya kuwa iwapo kutakuwa na dalili zozote za uvunjaji wa Amani inaweza kupelekea kusitisha shughuli zote za uchimbaji na kuwataka wachimbaji,wamiliki wa Leseni na wamiliki wa Mashamba kuheshimu Sheria za nchi na badala yake wasubili mgogoro huo utatuliwe na Baraza la ardhi la Wilaya.

 


 

Post a Comment

Previous Post Next Post