Mkurugenzi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Bw. Asangye Bangu, amewataka waendesha maghala kuzingatia uadilifu, uwajibikaji na utoaji wa huduma bora ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.
Akifungua kikao maalumu cha waendesha maghala kilichofanyika mjini Morogoro Julai 1, 2026, Bangu, amesema waendesha ghala wanapaswa kuendana na wakati kwa kuwa waadilifu, kutoa huduma zenye viwango vya juu na kuhakikisha mfumo wa stakabadhi za ghala unaendelea kuwa na tija kwa wakulima, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla.
Ameongeza kuwa maazimio na maelekezo yaliyotolewa katika kikao hicho yatawasaidia waendesha ghala kuongeza ufanisi wa kazi zao na kuendelea kutoa huduma bora kwa wadau wote wa sekta ya kilimo.



Post a Comment