WATUMISHI SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA WASHIRIKI KIKAMILIFU MEI MOSI, 2026 JIJINI DODOMA

Baadhi ya Watumishi kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Makao Makuu na Kanda ya Kati wameshiriki maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani 2026 katika Mkoa wa Dodoma yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Jamhuri tarehe 1 Mei, 2026 ambapo Mgeni Rasmi alikua Mkuu wa Mkoa huo Bi. Rosemary Senyamule.

‎Kitaifa Maadhimisho hayo yamefanyika mkoani Njombe ambapo Mgeni Rasmi alikua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

‎Maadhimisho ya mwaka huu yaliambatana na Kauli Mbiu: “Kazi zenye Staha ni Nguzo Imara kwa Maendeleo endelevu katika Utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050.”.





Post a Comment

Previous Post Next Post