‎MAADHISHO YA SALIKI YAFANYIKA KATA YA ZUZU,ELIMU YA LISHE YATOLEWA ‎

 


‎Maadhimisho ya Afya na Lishe (SALIKI) yamefanyika katika Kata ya Zuzu ambapo elimu ya matumizi ya lishe bora yalitolewa kwa wananchi lengo likiwa ni kuhakikisha jamii inatambua umuhimu wa lishe kwa ustawi wa afya bora.

‎Akizungumza na wananchi waliojitokeza kupata elimu hiyo katika Zahanati ya Zuzu, Diwani wa Kata ya Zuzu, Jenesta Malingo alisema kuwa upo umuhimu mkubwa wa mama mjamzito na watoto kupata lishe bora ili kutengeneza jamii yenye watu walio na afya bora. "Ndugu zangu nawapongeza kwa kujitokeza mahali hapa ili kupata elimu ya lishe. Huu ni muendelezo na tutaendelea kushirikiana ili kuhakikisha jamii yetu inaimarika kiafya. Tuzingatie haya tunayoelekezwa kwasababu msingi imara wa afya unaanzia huku tulipo" alisema Malingo.


‎Naye, Afisa Mtendaji wa Kata ya Zuzu, James Hans alisema kuwa wataendelea kuzingatia utoaji wa elimu ya lishe kwasababu suala la lishe bora ni mtambuka na haliepukiki.

‎Katika hatua nyingine, Muuguzi katika Zahanati ya Zuzu, Juma Nyala alieleza kuwa anayo furaha kuona mwitikio mkubwa wa wananchi kujitokeza kupata elimu ya lishe. "Nimefurahi kuona wananchi wanajali wito huu kwasababu ni kwaajili ya kuboresha afya zao na familia. Kwa mfano mana mjamzito akipata lishe bora atajifungua mtoto mwenye afya njema na akiendeleza utamaduni huo wa kuzingatia  lishe atakuwa amejihakikishia mtoto mwenye akili na imara kiafya" alisema.

‎Maadhimisho hayo yalihusisha utoaji elimu ya lishe kuhusu makundi ya vyakula, matunda na mbogamboga, upimaji uzito watoto na wajawazito na pia upishi wa vitendo wa uji ulifanyika ili kuonesha namna bora ya kupika uji wa lishe.


Post a Comment

Previous Post Next Post