DODOMA GLAM GIRLS WAFARIJI WANAWAKE HOSPITALI YA MIREMBE


Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, kikundi cha Dodoma Glam Girls kimetoa msaada kwa wanawake wenzao wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Mirembe, jijini Dodoma

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Mwenyekiti wa kikundi hicho, Happiness Njamasi, amesema lengo la msaada huo ni kuwafariji na kuwasaidia wanawake wenzao waliolazwa hospitalini hapo, ili kuwapa faraja na kuwafanya wajisikie kuthaminiwa katika kipindi hiki cha maadhimisho ya siku ya wanawake

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Dodoma Glam Girls, Juliana Kilua, amewaeleza waandishi wa habari kuwa misaada hiyo imepatikana kupitia michango iliyokusanywa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za kikundi hicho cha Dodoma Glam Girls



Naye Mhasibu wa kikundi hicho, Harieth Ndugulu, ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia chochote walicho nacho pamoja na kujiunga na kikundi hicho ili kuendelea kusaidia jamii, hususan wanawake wenye uhitaji

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yamekuwa fursa kwa makundi mbalimbali kuonesha mshikamano na kusaidia jamii, hasa makundi yenye uhitaji maalum.

Post a Comment

Previous Post Next Post