ALEX MSAMA ASAKWA NA TAKUKURU /DONGE NONO KUTOLEWA ATAKAYE TOA TAARIFA ZAKE

 


TAKUKURU imetangaza donge nono kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kumpata Alex Msama, ambaye anatajwa kuhusika katika tuhuma za vitendo vya rushwa na kukwepa mkono wa sheria.


Kwa mujibu wa taarifa ya taasisi hiyo, Msama anatafutwa kwa ajili ya mahojiano na hatua zaidi za kisheria, huku wananchi wakihimizwa kushirikiana kwa kutoa taarifa sahihi na za siri zitakazowezesha kukamatwa kwake. TAKUKURU imeahidi kulinda usalama wa watoa taarifa wote.


Taasisi hiyo pia imeonya kuwa mtu yeyote atakayemsaidia mtuhumiwa kujificha au kukwepa sheria atachukuliwa hatua kali za kisheria, na kusisitiza kuwa mapambano dhidi ya rushwa yanahitaji ushirikiano wa jamii nzima.

Post a Comment

Previous Post Next Post