MITIHANI YA USAJILI, LESENI YA UUGUZI NA UKUNGA KUFANYIKA DISEMBA 19

 ‎   


‎Na Edward Winchislaus

‎Dodoma,

‎Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania, Bi Agnes Mtawa, ametangaza kuwa mitihani ya usajili na leseni kwa wataalamu wa uuguzi na ukunga itafanyika rasmi tarehe 19 Disemba, 2025 kote nchini.

‎Akizungumza na waandishi wa habari leo Disemba 17, 2025 jijini Dodoma, Bi Mtawa amesema mitihani hiyo inafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010, kifungu cha 6, ikiwa na lengo la kupima umahiri wa watahiniwa kabla ya kuruhusiwa kwenda kutoa huduma za uuguzi na ukunga kwa jamii.

‎“Mitihani hii inalenga kupima umahiri wa kitaaluma kabla ya kumruhusu mtaalamu kwenda kutoa huduma kwa jamii ili kuhakikisha umma unapata huduma bora na salama za uuguzi na ukunga  kupitia kwa   wataalamu wenye  weledi na  umahiri,"amesema.

‎Amesema, jumla ya watahiniwa 4,414 wamekidhi vigezo vya kufanya mtihani huo na wamepangwa katika vituo sita vilivyopo mikoa mbalimbali nchini. Vituo hivyo ni Kampala International University (KIU) Dar es Salaam chenye watahiniwa 1,098, Tandabui Institute of Health Science and Technology (TIHST) Mwanza watahiniwa 971, St John’s University of Tanzania (SJUT) Dodoma watahiniwa 793, Ruaha Catholic University Iringa watahiniwa 720, IAA–Institute of Accountancy Arusha watahiniwa 549 pamoja na Tabora Polytechnic College chenye watahiniwa 283.

‎"Watahiniwa wamepangwa katika vituo hivi ili kurahisisha usimamizi na kuhakikisha mtihani unafanyika kwa ufanisi,” amesema.



‎Akiainisha kwa ngazi za elimu, Bi Mtawa amesema watahiniwa wa Astashahada ni 25 sawa na asilimia 0.6, Stashahada 3,713 sawa na asilimia 84, Shahada ya Uuguzi 625 sawa na asilimia 14, Shahada ya Ukunga 16 sawa na asilimia 0.4, huku Shahada ya Uuguzi katika utoaji wa dawa za usingizi na ganzi-tiba wakiwa 35 sawa na asilimia 1.

‎Aidha, amesema watahiniwa wote wanatakiwa kufika katika vituo walivyochagua siku moja kabla ya mtihani, yaani   Disemba 18, 2025 kuanzia saa mbili kamili asubuhi kwa ajili ya kupata maelekezo muhimu huku Siku ya mtihani, watahiniwa wanapaswa kufika kuanzia saa moja kamili  asubuhi bila kukosa.

‎“Yeyote ambaye hatofika kwa wakati siku ya mtihani atapoteza sifa ya kufanya mtihani huo,” amesisitiza.

‎Amefafanua kuwa mtahiniwa anatakiwa kuwa na kalamu nyeusi au penseli, picha mbili za pasipoti pamoja na kitambulisho halali huku  Kwa wale wasio na kadi ya indexing, wametakiwa kuwasilisha kitambulisho cha taifa, cha mpiga kura au leseni ya ude

‎Sambamba na hayo,Bi Mtawa amewakumbusha watahiniwa kuzingatia nidhamu, kuvaa kwa nadhifu, kufuata taratibu na kanuni za mitihani pamoja na kuheshimu maelekezo ya wasimamizi wakati wote wa mtihani huku akionya vitendo vya udanganyifu kabla, wakati au baada ya mtihani na kusisitiza kuwa ni kosa kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga ya mwaka 2010 kifungu cha 19(3), ambapo adhabu yake ni kufutiwa mtihani kwa mujibu wa kifungu cha 22 cha kanuni.

Post a Comment

Previous Post Next Post