CHRISTIAN BELLA APEWA URAIA WA TANZANIA



 Msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva wenye ladha ya R&B na Afro-pop, Christian Bella, amepewa rasmi uraia wa Tanzania.


Taarifa hiyo imetolewa leo Alhamisi, Desemba 18, 2025, jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, katika maadhimisho ya Siku ya Wahamaji Duniani.


Akizungumza kuhusu uamuzi huo, Simbachawene amesema Tanzania ina idadi kubwa ya wahamiaji na baadhi yao wamekuwa wakipewa uraia baada ya kukidhi vigezo.


> “Sasa anakwenda wapi? Amekwisha fika, ameoa hapa, ana watoto hapa na atapata wajukuu hapa. Anafanya kazi vizuri, hana makosa, amefuata utaratibu na muda wote alioishi hapa amelipa malipo stahiki, siyo wengine wanaolanda-landa tu,” amesema Simbachawene.


Aidha, Waziri huyo ameeleza kuwa uraia unaweza kufutwa endapo mhusika hatatii sheria na taratibu za nchi:


> “Hatuwezi kumpa uraia mtu ambaye ni hatari au anayegeuka kuwa hatari. Ndiyo maana kuna mchakato wa vetting unaofanyika kabla ya mtu kupewa uraia.”


Ikumbukwe kuwa awali Christian Bella alikuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), lakini ameishi Tanzania kwa muda mrefu akijishughulisha na shughuli za kisanii na kuchangia maendeleo ya muziki wa nchi.


Post a Comment

Previous Post Next Post