Na Suzana Alex
Mjumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) halmashauri kuu wilaya ya Dodoma mjini Mussa Luhamo amewaasa watanzania kuchagua viongozi wenye sera na mipango madhubuti ambayo italeta matokeo kwa vizazi vijavyo.
Amesema hayo alipokua Akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dodoma na kueleza kuwa mipango madhubuti ndiyo iletayo maendeleo ndani ya taifa.
"Niwaase vijana lakini niwaase watanzania kwa ujumla tuangalie sera na mipango itakayoishi kwa miaka mitano lakini itakayokuwa na matokeo kwa miaka na vizazi vyetu vinavyokuja,"amesema Luhamo
Kwa upande wake mgombea udiwani kata ya Nzuguni jimbo la Mtumba kupitia chama hicho,Leonard Ndama ahaidi kushirikiana na wananchi kutatua kero zinazowakumba.
Akizungumza kwenye mkutano wa kujinadi uliofanyikia katika kata hiyo amesema maendeleo hayaji yenyewe bali yanahitaji ushirikiano baina ya viongozi na wananchi wa eneo husika.
"Zipo changamoto mbalimbali zilizopo ndani ya kata yetu naahidi tunakwenda kuzitatua kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau wa maendeleo,"amesema Ndama

Post a Comment