Na Suzana Alex
Afisa Elimu wa kata ya Nzuguni iliyopo jijini Dodoma Mwl.Ayubu Seif awasihi wazazi kuepuka kuwatuma watoto kwenye maeneo ambayo si salama hasa kwenye vilabu vya pombe.
Akizungumza kwenye mahafali ya darasa la Saba katika shule ya msingi Ilakoze iliyopo jijini hapo Septemba 26 Afisa huyo ambaye pia alikua mgeni rasmi amesema wazazi wanapaswa kuwalinda watoto waliomaliza elimu ya msingi hasa katika kipindi hiki cha mpito.
"Mkiwa mnasubiri machaguo mliokua mmechagua niwaombe mkatulie nyumbani acheni kuzurura hovyo pia wazazi msiwatume watoto kwenye maeneo ambayo si salama kwao hasa kwenye vilabu vya pombe.
Aidha amewasihi wahitimu hao"Msiache kuwasaidia wazazi wenu kazi katka kipindi hiki cha kusubiria matokeo na kuzingatia masomo yenu ili muweze kutimiza ndoto zenu,"amesema Seif
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hiyo Olipa Mkuyu amewashauri wazazi kuwaepusha watoto na makundi yasiyofaa kwani makundi hayapo shuleni bali yanapatikana mitaani ambapo watoto ndipo wanapotokea.
Amesema wanaomba wazazi waendelee kuwaweka watoto katika njia sahihi pindi wanaporejea majumbani baada ya masomo.
"Muwasaidie watoto kufanya vitu ambavyo ni vya manufaa kwao ikiwezekana kuwaepusha na vipindi vya runinga visivyokua sahihi kwao pia kuwaepusha watoto na makundi yasiyofaa wanapokua nyumbani," amesema Mkuyu



Post a Comment