‎TCDD YAENDELEZA USHIRIKIANO NA SERIKALI,YASHAURI UWAZI KATIKA DENI LA TAIFA

 


‎Na Edward Winchislaus.

‎Taasisi ya Mtandao  wa Madeni nchini ( TCDD) imesema inaendelea kushirikiana  kwa ukaribu na serikali kupitia Wizara ya fedha na wizara ya mipango ili kuhakikisha mikopo inayokopwa na serikali inajibu changamoto za kimaendeleo hapa nchini.

‎Hayo yameelezwa septemba 23.2025 jijini hapa Dodoma na Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi hiyo Mhe.Godlisten Moshi  wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mkutano wa majadiliano kuhusu mikopo na maendeleo na fursa,changamoto zilizopo kwenye mikopo ya deni la Taita uliyowakutanisha kwa pamoja wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini na wawakilishi wa serikali kutoka wizara mbalimbali.

‎Amesema Taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 2000 wakati wa kampeni za madeni iliyoongozwa na Taasisi za kidini  ambapo kwa sasa Taasisi hiyo imeendelea kupanuka na kuongeza wadau   mbalimbali wakiwemo 'CSOs' wanaofatilia deni la Taifa.

‎" Taasisi mama ni Jumuiya ya wakristo Tanzania ,Baraza la maaskofu katoriki  Tanzania (TEC) pamoja na BAKWATA  lakini pia mtandao umeendelea kupanuka na kupata wadau wengi wanaopenda kufuatilia deni la Taifa  kutokana na kampeni ile ilizaa taasisi hii na baada ya taasisi hii kuzaliwa imekuwa ikifanya kazi kwa kushirikiana na wizara ya Fedha na mipango ili kuhakikisha kwamba ukopaji wetu unajibu changamoto za maendeleo nchini mwetu.

‎"Suala la ukopaji halikwepeki wala kuepukika na sisi kama nchi inayoendelea tunakopa na nia kubwa ya kukopa ni kuweza kuwaletea maendeleo wananchi,mtandao huu kazi yake kubwa ni kuangalia namna ya ukopaji ili tuwe na ukopaji wenye uwajibikaji ndani yake tunakopa nini ?,tunakopa wapi ? na tunakopa kiasi gani ? na mkopo huu unafanya shughuli gani hasa!!,"amesema Moshi.

‎Aidha amesema TCDD inaishauri serikali  na Taasisi zote zinazo simamia miradi mikubwa ya maendeleo kuwa na uwazi wa kutosha kwa jamii na  kuvitumia  vyombo ambavyo vinapitisha sheria na vile vyenye kazi ya kuisimamia serikali kama bunge ili viweze kutekeleza kwa uadilifu mkubwa kwani mikopo hiyo inapaswa kulipwa siyo misaada.

‎"Tunatoa wito kwa serikali  kuvitumia vyombo vinavyotekeleza viweze kutekeleza kwa uadilifu ili ifamike kwamba ni mikopo siyo misaada na kila mmoja wetu analipa na kila mwananchi anawajibu wa kufuatilia nini kimekopwa,kimekopwa wapi nini kinapaswa kurudishwa , kinakwenda kufanya kazi gani ili niende kufuatilia mradi husika uwezekuleta matunda yaliyokusidiwa ili  tusiendelee kukopa kila wakati katika jambo lile lile moja,"amesema.

‎Kwa upande wake mhadhili mwandamizi wa uchumi chuo kikuu cha Dodoma ( UDOM) Dkt.Lutengano Mwinuka amesema serikali imekuwa ikikopa kwa lengo la kuwezesha shughuli mbalimbali za kiuchumi  na kuhudumia miradi ya maendeleo  huku akiishauri serikali kuangalia maeneo mengine ya kukopa mikopo isiyokuwa na masharti magumu na riba kubwa ili kupunguza deni la Taifa.

‎Amesema ili deni la Taifa lisiendelee kukua serikali hainabudi kuzingatia madeni hayo kwa ujumla na kuhakikisha fedha hizo zinatumika kutekeleza miradi itakayo chochea ukuaji wa uchumi kama 'SGR' ili inapo lipa deni hilo na miradi iendelee kuzalisha fedha na kukuza uchumi zaidi pamoja na kupata vyanzo vingine vya fedha nje ya mikopo ya taasisi za kibiashara pamoja na kuongeza umakini kwenye miradi ya ubia.

‎"Tumekuwa tunakopa ili kutekeleza miradi ya maendeleo kubwa la kuangalia ni ustahimilivu wa deni la Taifa kuangalia kile unachokikopa na mapato ya Taifa,masharti yakiwa nafuu inatoa tafsiri nzuri namna gani deni utaweza lihudumia,tunatoa ushauri zaidi kuangalia maeneo mengine ya ambayo yanaweza kutuletea fedha na yakawa hayana masharti magumu zaidi mfano tunaona miradi ya ubia imeanza kuja inamikopo ndani yake lakini haina mizigo mikubwa kwa seeikali zipp njia nyingi mbadala ambazo zikizingatiwa tutapunguza deni la Taifa,"amesema Dkt.Mwinuka.

Post a Comment

Previous Post Next Post