CHAWATA DODOMA WATAKIWA KUEPUKA MIGOGORO

 


Na Suzana Alex

MWENYEKITI wa  Chama cha Watu wenye ulemavu Mkoa wa Dodoma (CHAWATA) Mchungaji Kelebi Mhawi amewataka viongozi wanaochaguliwa kwenye nafasi mbalimbali za chama hicho ,kujiepusha kunyosheana vidole na kulumbana, badala yake watumie muda huo kufanya kazi itakayoleta mabadiliko ya kiuchumi ili kuondokana na hali ya utegemezi.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti huyo alipokuwa akifunga mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa Chama hicho kwa ngazi ya mkoa uliofanyika Dodoma.

Mhawi amewataka viongozi hao kutumia muda wao mwingi katika kufanya kazi ikiwemo na kuwahamamsisha wana chama wao kujiunga kwenye vikundi, ili waweze kupata mikopo ambayo itakayowaletea mabadiliko ya kiuchumi ambao utaweza kuwaondolea hali ya kuwategemea zaidi wahisani.



Amesema  badala ya kutumia muda mwingi kulaumiana na kunyosheana vidole viongozi hao wanatakiwa kuwajibika katika kuhakikisha wanachama wao wanajishughulisha kwa kufanya kazi mbalimbali kwa ajili ya kujiletea mapato ambayo yatakayoweza kuwapunguzia kwenye changamoto zinazowakabili.

“Niwaombe viongozi wezangu mliochaguliwa unganisheni mawazo nyenu kwa pamoja kwa ajili ya kuangalia shughuli zenye tija ambazo zitakazoleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wanachama na hata kwa chama chenyewe, ili tuondokane na dhana iliyojengea kwa baadhi ya watu kuwa sisi ni watu wa kutegemezwa na misaada tu na sivyo vinginevyo”amesema Mhawi

Mwenyekiti huyo pia amewataka wanachama wa Chama hicho cha Chawata kuhakikisha wanalipa ada zao za uwanachama ili kukiwezasha kujiendesha chenyewe kiuchumi ,badala ya kutegemeza zaidi michango kutoka kwa wafadhali.



Naye mjumbe wa Mkoa wa Chama hicho Bashiru Kajuna akizungumza baada ya kuchaguliwa amesema kuwa watahakikisha wanawahamasisha wanachama kuungana ili waweze kupatiwa mikopo ambayo itakayowawezesha kufanya kazi za ujasirimali,ili waondokane na tabia ya kutegemea kuombaomba kwa ajili ya kupatiwa misaada kutoka kwa raia wema.

Kajuna amesema kuwa kwenye uongozi wao ambao uliochaguliwa watahakikisha hali ya utegemezi unaondoka kwa watu wenye ulemavu,kwa kuunda vikundi kwenye matawi yao yote yalipo ndani ya Mkoa huo ili waweze kupata mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Halmashauri za wilaya.

“Tutahakikisha wanachama wetu wanaunda vikundi kwa lengo la kuondokana na hali ya utegemezi wa kutembeza bakuli kwa ajili ya kuomba omba wakati serikali kupitia Halmashauri zake zote inatoa fursa za mikopo kwenye makundi mbalimbali ikiwemo ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu”amesema Kajuna

Kwenye uchaguzi huo uliosimamiwa na Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye ulemavu Mkoa wa Dodoma Justus Ngw’antalima,viongozi waliochaguliwa ni pamoja na Mwenyekiti Mchungaji Kalebi Mhawi,Makamu Mwenyekiti Mlemele Kavindo,Katibu Denis Nguruse,Katibu msaidizi Sospeter Chagondera,Mtunza hazina Abudula Mahundukila na msaidizi Maritina Bayo pamoja na wajumbe.

Ngw’antalima amewataka viongozi waliochaguliwa kutojivunia madaraka waliyopewa kwa dhamana ya kuaminiwa na wanachama wao,bali wakawatumikie kwa malengo ya kuwaondoa kwenye hali ya umasikini na hatimaye kufikia hatia ya kujitegemea wao wenyewe badala ya kusubiri kusaidiwa na watu wema.

“Mmechaguliwa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu wanataka kuona cheche za moto wa mabadiliko unakuwepo na ndani ya uongozi wao hatimaye unaona moto ukiwaka,badala ya kujivunia na vyeo hivyo mlivyokabidhiwa na wanachama wenu,naomba mkalete mabadiko ndani ya chama na kwa watu wenu mliopewa mkawaongoze kiuchumi zaidi”amesema Ngw'antalima

Aidha Katibu huyo amewataka viongozi hao kushirikiana na vyama vingine ambavyo vipo ndani ya shirikisho hilo,kwa kufanya kazi ambazo zitakazoleta maendeleo ya kiuchumi kwa kila mlemavu ili kuondokana na hali ambayo inayodhaniwa kuwa walemavu ni watu wa kukaa barabarani na kupita mitaani kwa ajili ya kuomba.

Amesema wakishirikiana kwa pamoja na vyama hivyo vilivyomo kwenye shirikisho wataweza kuanzisha miradi mbalimbali na hatimaye wakapatiwa mikopo kutoka taasisi za kifedha na kuwawezesha  kujiinua kiuchumi kwa kupitia mitaji yao na ha

Post a Comment

Previous Post Next Post