zi
Na Peter Mkwavila DODOMA
MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) zimezionya taasisi zisizo za kiserikali zinazotoa elimu ya usalama barabarani ambazo zinazotumia nafasi zao kujipatia fedha za udanganifu.
Onyo hilo limetolewa na Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Ardhini Ezekiel Emmanuel alipokuwa akizungumza na Mabalozi wa Usalama Barabarani mkoa wa Dodoma.
Emmanuel alisema kuwa bado kuna changamoto kwa baadhi ya taasisi zinazotoa elimu ya usalama barabarani wanatoa elimu hiyo kwa malengo yao binafsi ili waweze kujipatia fedha kwa njia ya rushwa badala ya malengo halisi.
Alisema kuwa miongoni mwa taasisi hizo baadhi yao wamedhubutu kutumia majina taasisi mbalimbali kama vile Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini,Tanroad na Tarura ili waweze kuaminiwa wakati siyo kweli.
"Zimekuwa zikijinadi kwa kujitambulisha kuwa wanafanya kazi kwa kushirikiana na taasisi hizo,wakati siyo kweli na wanafanya hivyo ili waweze kujipatia fedha kutoka kwa wadau na jamii.
"Wengi wamekuwa wakitumia majina ya taasisi hizo za kiserikali ikiwemo Latra kwa kizingizio cha kuelimisha jamii elimu ya usalama barabarani wakati hakuna mkataba wowote unaoonyesha makubaliano hayo
Akizungumza na mabalozi hao wa usalama wa barabarani (RSA),aidha amewaomba kutumia nafasi yao kutoa elimu sahihi kwa jamii inayowazunguka ili wawe na ufahamu wa usalama wao.
Alisema kuwa wakifanya hivyo watasaidia jamii katika kutambua haki zao wanazotakiwa kizipata kupitia kwenye vyombo vya usafiri na hata kwenye matumizi ya barabara.
Naye Mwenyekiti wa taasisi hiyo ya Mabalozi wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma John Luganga akizungumza kwenye ziara hiyo ameziomba taasisi na wadau zinazojihusisha na elimu zinatakiwa kuaminiwa na watoa maamuzi.
Aidha ameiomba serikali pia,kuwachukulia hatua za kisheria kwa wanaotoa elimu mbalimbali ya utoaji huduma za barabarani ambao siyo waaminifu kwa kuwa wanaharibu maadili ya utendaji wa kazi.
Aidha alisema kuwa wao kama mabalozi kazi yao ni kuimarisha mahusianao baina ya taasisi na mamlaka za usimamizi ili kuleta ufanisi wa utendaji ili jamii iweze kutambua usalama wa barabara ikiwemo na ulinzi wa miundombinu.
Katika ziara hizo Mabalozi hao walitembelea taasisi mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha mahusiano ikiwemo Ofisi ya Jeshi la zima moto na uokoaji,Latra,Tanroad,Tarura Tira na Ofisi ya RTO Dodoma.
MWISHO.


Post a Comment