Na Peter Mkwavila DODOMA
MAKAMU Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi Bara Stephen Wasira anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kongamano la maombi lililoandaliwa na Chama cha Maaskofu,Wachungaji Mitume na Manabii Tanzania kwa ajili ya kuombea Taifa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu wa 2025.
Pia kwenye Kongamano hilo litatumia nafasi hiyo kuvipongeza vyama vya siasa kikiwemo Chama cha mapinduzi kwa kuwateua wagombea wake kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika mwaka huu wa 2025 kwa nafasi Rais,Makamu wa rais,Rais wa Zanzibar na Chama cha Demokrasia na maendeleo kwa kuwapata viongozi wao.
Akizungumza na Wachungaji,Maaskofu,Mitume na Manabii Nchini na waandishi wa habari Dodoma Askofu Dk Mussa Mlawi,alisema kuwa kongamano hilo litafanyika Dodoma mwaka huu machi ambapo kutakuwa na maombi kwa ajili pia ya kuiombea Nchi,Rais pamoja na watendaji wake.
Dk Mlawi alisema,Taifa mwaka huu Watanzania tunaenda kufanya uchaguzi mkuu ambao vyama mbalimbali vya siasa vitashiriki kugombea nafasi ya Urais,Ubunge na Madiwani,hivyo Kongamano hilo litafanya maombi ili ufanyike kwa amani,huru,haki,uwazi na utulivu.
Alisema kuwa ni muhimu kuombea uchaguzi huo mkuu na Taifa kwa ujumla ukizingatiwa kuwa mwaka huu tunaenda kutumia demokrasia yetu ya kuwachagua viongozi tunaowahitaji kutuongoza akiwemo Rais,Wabunge na Madiwani.
Rais huyo amewaomba Watanzania nchini kote kuendelea kuliombea Taifa na kuhakikisha wanajitokeza kujiandikisha kwenye daftari la uchaguzi huo,pamoja ambao tunaamini kama chama utakuwa wa amani,haki,huru na utulivu.
Alisema kuwa,pamoja na maombi hayo Chama hicho cha Wachungaji maaskofu manabii na mitume,pia kitatumia Kongamano hilo kuwahimiza vijana wenye sifa na wito wa uongozi wajitokeze kugombea nafasi za ubunge na udiwani.
"Chama kitatumia kongamano hilo kuwahamasisha vijana kote nchini kwa wale wenye wito kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi hizo,kwa kupitia watumishi wa mungu ili vijana hao wajitokeza na kuziomba ili na wao waweze kuwa viongozi"alisema
MWISHO.


Post a Comment