VYOMBO VYA HABARI VIMETAKIWA KURIPOTI MABADILIKO YA TABIANCHI NA ATHARI ZAKE KWA JAMII

 


Na Edward Winchislaus.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na michezo Mhe.Prof.Paramagamba John Aidan Mwaluko Kabudi ( Mb) amevitaka vyombo vya habari kote nchini kutenda usawa kwa vyama vya kisiasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa 2025 ili kuepusha machafuko ya amani nchini.

Wito huo ameutoa leo Februari 13.2025 katika mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini unaoendelea jijini hapa Dodoma na kutarajia kuitamatika kesho Februari 14 mwaka huu,ambapo amesema kuwa vyombo vya habari vinapaswa kutoa habari za usawa kwa vyama vyote vya kisiasa.

Amesema kuwa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari kwa kila nyanja ili kuhakikisha vinazidi kutoa taarifa sahihi kwa wananchi na jamii kiujumla.

"Maadhimisho ya siku ya redio Duniani yanaenda sambamba na mkutano wa mwaka wa vyombo vya utangazaji nchini unao wakutanisha waandishi wa habari mbalimbali na kubadilisha mawazo katika tasnia ya habari,nivitake vyombo hivi vya habari vitende usawa katika kipindi hiki cha uchaguzi kwa vyama vyote vya kisiasa.

"Ahadi yangu kwenu mimi na wizara ninayo iongoza itawapa ushirikiano mnaouhitaji kwa kila shemu,katika habari,utamaduni,sanaa na michezo,"amesema



Aidha Prof.Kabudi amesema kutokana na uwepo wa mabadiliko ya tabianchi nchini vyombo vya habari havinabudi kuendelea kutoa taarifa za mara kwa mara juu ya mabadiliko hayo pamoja na athari zake kwa jamii ambapo ameeleza kuwa huathiri kwa ukubwa shughuli za kijamii ikiwemo Kilimo.

" Mabadiliko ya Tabianchi yana athiri vitu vingi katika kipindi hiki ili wananchi wachukue tahadhari mapema redio kimekuwa chombo cha kwanza kuhabarisha wananchi juu ya mabadiliko hayo kwahiyo tunabidi kuwa na vituo vya redio vyenye vipindi vya tabianchi.

Katika hatua nyingine prof.Kabudi amewakumbusha waandishi wa habari hususani watangazaji wa vyombo vyote vya habari kuwa na matumizi sahihi na fasaha ya  lugha ya kiswahili na kingereza pindi wanapo wasilisha taarifa zao kupitia vyombo hivyo ili kutoibananga lugha ya kiswahili.



Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasilisno Tanzania TCRA Dkt.Jabiri Kuwe Bakari amevitaka vyombo vya utangazaji nchini kutoa nafasi ya utabili wa hali ya hewa katika vipindi vyao vya redio na Televisheni.

Post a Comment

Previous Post Next Post