Na Edward Winchislaus
WAZIRI wa nchi ofisi ya waziri mkuu kazi vijana,Ajira na wenye ulemavu Mhe.Ridhiwani Kikwete amesema serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo na sekta binafsi unaolenga kuimarisha ushiriki na michango ya wanawake na wasichana katika masomo ya sayansi ambapo imeanza utekelezaji wa sera ya Elimu na mafunzo toleo la mwaka 2023 sambamba na mitaala iliyorekebishwa ambapo serikali imeweka msukumo katika kuandaa walimu bora na kuweka mazingira wezeshi katika kujifunza na kufundisha makundi yote likiwemo kundi la wanawake na wasicha.
Hayo ameyaeleza leo feburuari 11,2025 katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya kikwete jijini hapa Dodoma ambapo amesema kuwa kutokana na ugumu wa uwepo wa elimu shindani nje ya Taifa letu hivyo eneo hilo halinabudi kuangaliwa kwa ukaribu ili sera hiyo ijikite katika utatuzi wa changamoto hizo.
Pia amesema kuwa kupitia chuo kikuu cha uliya Tanzania serikali imeendesha programu ya mafunzo kwa mwaka mmoja inayolenga kuonesha sifa ya kujiunga na Elimu ya juu katika nafasi ya STEM kwa wanawake na wasichana wanaotoka katika kaya zenye kipato cha chini ambapo mwaka 2024/25 wanafunzi wapatao 176 kati ya wanafunzi 188 waliyofaulu mitihani ya mwisho ya programu husika na kudailiwa na Taasisi mbalimbali kisha kujiunga na Elimu ya juu nchini.
"Kiwango cha kundi la wanawake na wasichana wanaoshiriki kazi za STEM duniani zinakadriwa kuwa asilimia 33 pekee kwa upande wa Tanzania kiwango cha kundi hili kinachokadriwa kufanya kazi za STEM kinakadriwa kufika asilimia 36 kutokana na ushiriki wake mdogo nchi mbalimbali duniani ikiwemo Tanzania zinatekeleza juhudi mbalimbali zinazolenga kuweka mazingira wezeshi wakumotisha ushiriki wa wanawake na wasichana katika kazi za STEM",amesema Kikwete.
Pia ameongeza kuwa ufadhili wa masomo kupitia bodi ya mikopo ya masomo ya elimu ya juu ambao unatoa upendeleo kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kama vile Uhandisi .
Aidha amesema serikali imeanzisha furusa mbalimbali kupitia bodi hiyo zinazolenga kuhamasisha vijana wa kitanzania Ikiwemo wasichana kujiunga na fani ya sayansi ambapo ameeleza kuwa furusa hizo zinajumuhishwa katika samia scolar ship inayotoa ufadhili kwa wahitimu wa kidato cha sita wanaojiunga na sayansi na kufaulu vizuri hudusani katika Tiba na uhandisi hisabati.
" Katika maaka 2024/ 25 jumla ya wanafunzi Wasichana 260 wamepatabufadhili wa masomo ya tiba,uhandisi na Hisabati kupitia samia scolar ship.
Sambamba na hayo ameeleza kuwa serikali imeendeleza kuzihimiza shule na vyuo nchini Kuweka mazingira wezeshi ya kufundishia na kujifunza kwa wanafunzi Wasichana na wanawake.
Aidha amesema kuwa serikali inatambua na kuthamini mchango wa wadau wa maendeleo na sekta binafsi nchini katika kuhamasisha nguvi ya wanawake na wasichana katika STEM


Post a Comment