KATABAZI:TUMEMKAMATA BAKARI KWA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA AINA YA MIRUNGI

 



Na Edward Winchislaus.

Jeshi la polisi mkoani Dodoma linamshikilia Omary Bakari ( 45) kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya  aina ya mirungi Klg.148 kinyume na sheria kwa kutumia gari  T120ABF aina ya Canter ( kenta)  ambalo ndani yake linachumba maalumu cha kuficha dawa za kulevya.



Hayo yameelezwa leo Februari 10,2025 na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Dodoma SACP George Katabazi wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini hapa Dodoma ambapo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa Februari 4 mwaka huu katika Wilaya ya Chemba kufuatia oparesheni ya jeshi hilo.


Pia amesema kuwa wamemkamata Juma Hamza maarufu Majambazi ( 27) akiwa na wenzake sita wenye umri kati ya 20 hadi 30 kwa tuhuma za kuwajeruhi watu watatu ambapo ameeleza kuwa vijana hao ni mtandao wa waharifu unaojulikana kama maronjoo wanao jihusisha na uharifu mbalimbali ukiwemo wizi ,ubakaji na unyanganyi wa kutumia silaha.


"Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma tunaendelea na oparesheni katika maeneo mbalimbali mkoa wa Dodoma,ambapo 4/2/2025 tulimkamata Omary Bakari mwenye umri wa miaka 45 kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya Klg.148 kinyume cha sheria alikuwa akisafirisha dawa hizo kwa kutumia gari T220  ABF aina ya kenta kinyume cha sheria,gari hilo limetengenezwa au linachumba maalumu cha kuifadhi dawa hizo ili msafirishaji asiweze kabainika.


"Pia tumemkamata Juma Hamza maarufu majambazi 

huyu anamiaka 27 akiwa na wenzake 6 hao vijana wanaumri kati ya miaka 20 hadi 30 tuliwakamata kwa tuhuma za kuwajeruhi watu watatu na vijana hawa ni mtandao wa uharifu wanajihusisha na uharifu mbalimbali kama wizi ,unyangani wa kutumia slaha na ubakaji",ameeleza SACP Katabazi.


Katabazi ameongeza kuwa wameendelea na upelelezi wa kusafirisha madawa ya kulevya pamoja na waharifu wa ubakaji na unyanganyi kwa kutumia silaha ili hatua nyingine za kisheria zizidi kuchukua mkondo wake.



Aidha jeshi la polisi mkoani Dodoma limetoa onyo kali  kwa wanaojihusisha na vitendo vya uharifu kuacha mara moja kabla hawajachukulia hatua kali za kisheria dhidi yao.

Post a Comment

Previous Post Next Post