TAASISI YA PST YATOA MAFUNZO YA USTAARABU NA ITIFAKI KWA WADAU SEKTA MBALIMBALI KUTOKA MIKOA 19 KWA BARA NA VISIWANI..

 



Na Deborah Lemmubi-Dodoma.


TAASISI ya Protocol Service Team (PST) chini ya Mkurugenzi wake Ndugu Hussein Abbakari Hussein imeendelea kutoa Mafunzo ya Itifaki na Ustaarabu kwa Sekta mbalimbali ikiwamo Watumishi wa Ofisi za Mikoa,Walimu, Madaktari  na Viingozi wa Dini. 


Akifunga Mafunzo hayo ya Itifaki na Ustaarabu Mhe Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ametoa shime kwa Washiriki wa mafunzo hayo  kuwa matendo na maneno yao sasa yakaoneshe kuwa wao ni watu tofauti ambao tayari wamekwishapata Elimu hii mpya na sio wapate elimu lakini mabadiliko yasiwepo kwao.



Senyamule ameyasema hayo mapema Leo hii Jijini Dodoma Januari 26,2025 wakati akifunga Mafunzo ya Ustaarabu na Itifaki yaliyoratibiwa na Taasisi ya Protocol Service Team.



Na kuongeza kuwa elimu hii ikawasaidie kubadilika kwani wameshapata kujua kipi ni kitu sahihi na hii itatokana na dhamira yao ya dhati ya kuchukua hatua na kutaka kubadilika.



"Hapa niendelee kutoa shime madam mmejifunza, maneno yenu yaoneshe ninyi tayari mna elimu mpya,matendo yenu yaoneshe nyi ninwatu wengine sio ukae hapa kwa siku zote halafu tuone mambo yako hayana mabadiliko".



"Nataka kusema kuwa msione mmesoma leo mkaona mmeshamaliza ,hiyo ni hatua ya kwanza ya kubadilika kuwa sasa mnafahamu kitu sahihi nikipi lakini kuamua kukifanya inatikana na dhamira yako ya kuchukua hatua ya kubadilika kunataka dhamira ya dhati".


Aidha Senyamule amesema wapo baadhi wanaodhani kuwa suala la ustaarabu na kustaarabika kunakuja tu kitu ambacho sio kweli kwani Ustaarabu unafundishwa kama wao walivyoamua kusoma, na kutoa mfano kuwa inaweza jengwa majengo mazuri lakini kama watu hawakufundishwa namna ya kuyatunza hayatadumu na kufurahi kuona kujifunza kwa Ustaarabu kumeongezeka.


"Ustaarabu unafundishwa kama nyie ambavyo mmeamua kusoma,kwahiyo Ustaarabu watu wengi wanafukiri ni kitu kinakuja chenyewe,nafurahi sasa upana wa watu kujua kumbe Ustaarabu nao ni kitu cha kujifunza umeongezeka ,kama ninyi hapa Watanzania 110 tunaju mtaenda kustarabisha na wengine".



Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PST Tanzania Ndugu Hussein Abbakari Hussein ameeleza kuwa Mafunzo haya yalilenga kuboresha uelewa wa masuala ya Itifaki na Ustaarabu wa Kidiplomasia kwa Washiriki kutoka Sekta mbalimbali kwa Tanzania Bara na Visiwani. 


"Mafunzo haya yalilenga kuboresha uelewa wa masuala ya Itifaki na Ustaarabu wa Kidiplomasia kwa washiriki kutoka sekta mbalimbali,  tunafurahi kuona washiriki kutoka Mikoa 19 kwa Bara na Visiwani wakiwa wamejifunza somo hili muhimu,mafunzo haya yamehusisha washiriki kutoka makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma,Morogoro, Singida, Iringa na viongozi wa Dini pamoja na walimu".


Aidha Mkurugenzi huyo amebainisha mafanikio matatu ya mafunzo hayo kuwa ni pamoja na kuongeza maarifa na ujuzi wa washiriki, Kujenga mshikamano wa kijamii na Kitaasisi kwa Washiriki na kufungua fursa za kushirikiana kwa karibu kati ya washiriki hao.


"Mafunzo haya yameleta mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuongeza maarifa na ujuzi kwa washiriki na kuimarika katika masuala ya Itifaki mawasiliano rasmi na Ustaarabu wa Kidiplomasia,pili kujenga mshikamano wa kijamii na Kitaasisi kwa washiriki, Na tatu yamefungua fursa za kushirikiana kwa karibu zaidi kati ya washiriki kutoka sekta mbalimbali lwa lengo la kuimarisha Maadili ya Kitaaluma kwa jamii".



Sambamba na hayo yote pia Mkurugenzi huyo ametoa mapendekezo yao kama Taasisi kwa Mkuu wa Mkoa kuwa kutokana na umuhimu mkubwa wa mafunzo haya wanapendekeza kuwa mafunzo ya Itifaki na Ustaarabu wa kidiplomasia pia yafikishwe kwa Makatibu tawala wa Wilaya wa Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma pamoja na Maafisa Tarafa wa tarafa zote za Mkoa wa Dodoma kati ya mwezi wa tatu kuelekea kipindi cha Mwenge wa Uhuru.



Naye mmoja ya Wakufunzi wa Mafunzo hayo Dkt Godwin Amani Gonde ambaye ni Mhadhiri kutoka Chuo cha Diplomasia amesema ana imani kwamba elimu waliyopata washiriki hawa watashuhudia mabadiliko makubwa ambayo yatafanywa kwa vitendo kwani kwa siku zote za mafunzo washiriki wamepata kujifunza dhana ya Mwenge,kwenye somo la Itifaki na Ustaarabu wamejifunza maana halisi ya itifaki,umuhimu wa Itifaki katika maeneo ya kazi,namna ya kuweza kuongea kama Watumishi wa Umma,wamejifunza masuala ya Ustaarabu wa namna ya kuvaa,kula,namna ya kutii wakubwa wao na waliochini yao kwankuwaongoza. Vile vile wamejifunza falsafa ya Utu pamoja na Utanzania kuijua nchi yao,wamejifunza Sheria za Itifaki kujua nini kinatakiwa na ni wakati gani.



Ndugu Twaha Swalehe Kidabu ni mmoja ya Washiriki kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe yeye ametoa wito kwa vijana wa Kitanzania wafahamu kuwa Ustaarabu, Itifaki na Diplomasi ni gharama hivyo gharama hiyo wanaihitaji ili waweze kustaraarabika na pia ili waweze kuwa vyema katika Itifaki na diplomasia ni lazima wawekeze kwasababu kama mtu alishazoea kuenenda tofauti na Itifaki halafu akaja akaipata ile Itifaki,shida inakuwa sio kuisoma ila shida bali inakuwa ni namna ya kuyatumia yale maarifa aliyoyasoma ya Itifaki, Ustaarabu na Diplomasia kuyatumia katika maisha yake ya kila siku.


Na namna atakavyokuwa anabadilika ule mchakato wake ndo gharama kwasababu huenda kuna watu walishazoeana kutembea na kufanya yasiyo ya kistaarabu watamkimbia baaday ya kubadilika na wale waliomzoea kuona akifanya mambo ambayo sio ya kiitifaki watamkimbia kwasababu watamuona sio miongoni mwa watu wao tena.



Mafunzo haya yaliyofanyika Jijini Dodoma ni ya siku tatu na yamekuwa na washiriki takribani 110 kutoka Mikoa hiyo 19 kwa Tanzania Bara na Visiwani.

Post a Comment

Previous Post Next Post